Wednesday, January 6, 2016

WAZIRI WA KILIMO ATUA MKOANI IRINGA, AKUTANA NA WAKULIMA WA TUMBAKU

mwi5
Waziri wa Kilimo Mifugo na Ushirika Mh. Mwigulu Nchemba akipokelewa katika ofisi ya Mkuu wa Iringa na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa Mh. Amina Masenza na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh. Richard Kasesela.
mwi3
Waziri wa kilimo Mh Mwigulu Nchemba leo amesikiliza malalamiko ya wakulima wa Tumbaku na kuwahakikishia zao la tumbaku halitakufa kwani linaleta pato kwa taifa.

Waziri wa kilimo Mh Mwigulu Nchemba leo amesikiliza malalamiko ya wakulima wa Tumbaku na kuwahakikishia zao la tumbaku halitakufa kwani linaleta pato kwa taifa.
wakulima wamelalamika sana uchelewashwaji wa pembejeo, bei duni ikiwemo madaraja mengi ya mfano kuna madaraja zaidi 72 ya grade za tumbaku kitu ambacho wakulima wamesema inawaumiza sana kwenye bei.
Pia wakulima wamelalamika ubadhirifu wa chama cha mtandao (Union) kiitwacho ITCOJE. Katika ziara hiyo Mh waziri aliambatana na Mrajisi wa vyama vya ushirika Dr. Rutabanzibwa na Mkurugenzi wa bodi ya Tumbaku Bwana Mushi. Mh. waziri ameagiza matatizo mengi yawe yametattuliwa kabla kikao cha bunge hakijaanza.
Mh. Mwigulu aliwasili kwanza ofisi ya Mkuu wa mkoa na kupokewa na Mkuu wa Mkoa Mh Amina Masenza na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela. Mh Masenza alimpa taarrifa fupi ya hali ya Kilimo katika mkoa wa IRINGA.
mwi4
Wajumbe mbalimbali wa mkutano huo wakiwa katika mkutano
mwi2
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Ushirika akisalimiana na wajumbe mbalimbali wa mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake