Friday, January 8, 2016

WAZIRI WA NCHI TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ AFUNGUA MRADI WA MAJI MAKUNDUCHI MKOA WA KUSINI UNGUJA

jm1
Waziri wa Nchi Tawala za Mikoa na Idara Maalum Mh. Haji Omar Kheri akisalimiana na wafanyakazi wa Mamla ya Maji Zanzibar (ZAWA) mara baada ya kufika Kijiji cha Makunduchi kufungua mradi wa Miji ikiwa ni shamrashamra za kuazimisha miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
jm2
Waziri wa Nchi Tawala za Mikoa na Idara Maalum Mh. Haji Omar Kheri akifungua pazia pamoja na kufungua Maji kuashiria ufunguzi rasmin wa Mradi wa Maji safi katika Kijiji cha Makunduchi Mkoa kusini Unguja, ikiwa ni shamrashamra za kuazimisha miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

jm3 jm4
Tenki jipya la kuhifadhia Maji lililopo Makunduchi.
jm5
Baadhi ya wageni walikwa waliohudhuria katika ufunguzi wa Mradi wa Maji safi uliozinduliwa Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja ikiwa ni shamrashamra za kuazimisha miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
jm6
Waziri wa Nchi Tawala za Mikoa na Idara Maalum Mh. Haji Omar Kheri akizungumza na wananchi wa Makunduchi katika ufunguzi wa mradi wa Maji safi, ikiwa ni shamrashamra za kuazimisha miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Amewataka wananchi wa kijijihicho kushirikana na Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) ili kuendeleza miundo mbinu hiyo na piaamewata kuchangia kiasi cha pesa kwa wale watakao pata Maji. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake