Mkuu wa Idara ya Uchumi na Uzalishaji Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Ndaro Kulwijila (katikati), akiwakaribisha mkoani humo watafiti wa kilimo kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), ambao walifika ofisini kwake kujitambulisha kabla ya kwenda kutoa mafunzo kwa watafiti, wakulima na wadau wa kilimo kuhusu matumimizi ya kilimo cha bioteknolojia ambacho kinafanyiwa utafiti na watafiti wa kilimo kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech.
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiruguru kilichopo jijini Mwanza, Dk.Evelyne Lukonge (wa pili kulia), akifurahi wakati akisalimiana na Mtafiti Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia, Dk.Emmarold Mneney alipo wasili na maofisa wenzake watafiti katika ofisi yake kujitambulisha kabla ya kutoa mafunzo kwa watafiti wa kituo hicho na wadau wa kilimo. Kulia ni Mtafiti Kiongozi kutoka Costech, Dk.Nicholaus Nyange na wa pili kushoto ni Mratibu Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia Afrika, Daniel Utunge kutoka nchini Kenya.
Watafiti na washiriki wakiwa kwenye semina hiyo.
Semina ikiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Watafiti na washiriki wakiwa katika semina hiyo.
Washiriki wakifuatilia kwa karibu mafunzo hayo.
Mtafiti kutoka ARI -Ukiriguru, Maganga Joseph akiuliza swali katika semina hiyo.
Taswira ya ukumbi wa semina hiyo. |
Na Dotto Mwaibale, Mwanza
MTAFITI Kiongozi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) Dk.Ncholaus Nyange amesema Bioteknojia ya kilimo nchini itafanyiwa utafiti ili kukabiliana na changamoto ya mazao kuharibika.
Hayo aliyaelezwa jijini Mwanza katika semina ya siku moja ya Jukwaa la Bioteknojia iliyoandaliwa mahsusi kwa watafiti na wadau wa kilimo.
Alisema ni muhimu bioteknojia ya kilimo kufanyiwa utafiti ili kwenda sanjari ya dunia ya kilimo ambayo inahitahi watafiti.
Katika hatua nyingine Dk. Nyange amewataka wananchi na wataalamu mbalimbali kuthamini tafiti za kilimo za bioteknolojia zinazofanywa na watafiti wetu wa ndani badala ya kusikiliza propoganda za nje kuwa hazifai.
"Bioteknolojia au uandisijemi ni teknolojia ambayo inakubalika lakini kuna taasisi kadhaa za nje hazilali usingizi zinaeneza propoganda kuwa haifai wakati wao wanaitumia" alisema Nyange.
Alisema teknolojia hiyo inayotumika kwa kilimo cha pamba imeleta mafanikio makubwa katika nchi za Bakinafaso, India, Marekani na nyingine nyingi ambazo hivi sasa zimekuwa zikiongoza kwa utengenezaji wa nguo za kotoni duniani lakini nchi hizo zimekuwa mstari wa mbele kuzuia isitumike hapa nchini.
Mtafiti Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia, Dk.Emmarold Mneney alisema teknolojia hiyo mpya ambayo ina zaidi ya miaka 20 imesaidia kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi kutokana na kuwepo kwa ukame, magugu na wadudu waharibifu wa mazao na ndio maana wameamua kuipeleka kwa wakulima ili waijue.
"Tumeamua kuwafuata watafiti mikoani ili kuendesha mafunzo ya teknolojia hii mpya ambapo tumeanza hapa Mwanza na tutaenda Bunda na Butihama mkoani Mara na watu tuliowalenga ni watafiti wa kilimo, walimu ambao tunaamini wakiilewa nao watatoa elimu hiyo kwa makundi mengine" alisema Dk.Mneney.
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiruguru, Dk. Evelyne Lukonge alisema katika ukanda huo wa ziwa changamoto kubwa waliyonayo ni magonjwa ya mazao ya pamba, ndizi, viazi na mihogo hivyo njia pekee ni kwa watafiti kutumia teknolojia hiyo ili kuwa komboa wakulima.
Dk. Lukonge alisema changamoto nyingine kubwa ni fedha za kusaidia kufanya tafiti hizo ambapo aliiomba serikali kuliangalia suala hilo kwa karibu zaidi.
Mkuu wa Idara ya Uchumi na Uzalishaji Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Ndaro Kulwijila akiwakaribisha mkoani humo watafiti hao kutoka Costech alisema hivi sasa duniani hakuna kilimo kitakachofanikiwa bila ya kuwa na watafiti hivyo aliiomba serikali kutenga fedha za kutoka ili kuwawezesha watafiti kwa ajili ya kufanya tafiti mbalimbali za kilimo.
Kulwijila alisema mkoani humo changamoto kubwa waliyonayo ni kupanda kwa gharama kubwa ya kilimo cha pamba kwani bei yake imeendelea kuporomoka kutoka sh.1200 kwa kilo hadi kufikia sh. 800 hadi 700 jambo linalowakatisha tamaa wakulima.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
No comments:
Post a Comment