WANAWAKE KWA WANAUME HII NI FURSA YA KUKUSHIRIKISHA KATIKA MCHAKATO WA KISIASA UGENINI!
Matamaniyo yetu hapa ugenini hayataweza kutekelezwa bila sisi kutoa ushirikiano.
Tunapooneka ndipo tunapotambulika na tunapotambulika ndipo mawazo yetu na sauti zetu zitakapothaminiwa. Mchango wetu ni mkubwa na unatambulika, huu ni wakati ambao hatuwezi kurudi nyuma. Ni vyema kushiriki katika maamuzi yanayohusu uwepo na usalama wetu ugenini, matumizi ya kodi tunayochangia kuilipa, elimu kwa watoto wetu na kuandaa kizazi chenye sauti. Endapo tunayoyaona yanatukereketa ni muhimu kushiriki katika kuleta mabadiliko.
Ngugu zetu wa Hispanic hupewa kipaumbele kwa sababu ya kujishirikisha kwa kina kikubwa bila kubaki nyuma. Mchango wao hutambulika, matakwa yao hutimizwa kwasababu kura yao inahitajika, nasi pia tunaweza hilo.
Hivyo ndugu zangu naomba tushiriki kwa wingi, tuulize maswali na kuhamasisha mwamko kwa kizazi chetu kushiriki katika michakato ya kisiasa hapa nchini. Bila kushiriki katika michakato ya kisiasa hatutakuwa na sauti wala uwezo wa kupendekeza sera zitakazotuletea afueni. (wenzetu wa west wamo tayari na wanashiriki katika viti mbambali)
No comments:
Post a Comment