Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akiwasili katika Hospitali ya Mkoa wa Manyara.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akipata maelezo namna ya kitengo cha maabara ya Hospitali ya Mkoa wa Manyara inavyofanya kazi
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla amefanya ziara ya kikazi katika Hospitali ya Mkoa wa Manyara pamoja na Kituo cha Afya Magugu kilichopo Wilayani Babati ambapo ametoa maagizo mbalimbali ya kiutendaji na sera katika utoaji wa huduma kwenye sekta ya Afya nchini.
Dkt. Kigwangalla alianzia katika Hospitali ya Mkoa wa Manyara na kisha kuagiza uongozi wa Hospitali ya Mkoa wa Manyara kuwa na chumba maalumu cha kuwahudumia wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum ((ICU) angalau kuwa na vitanda viwili vya kuanzia.
Dkt. Kigwangalla alibaini changamoto mbalimbali licha ya kuwa na majengo machache na mapya, katika Hospitali hiyo inakabiriwa na ukosefu wa chumba cha wagonjwa hao mahututi hivyo kuagiza Katibu Tawala na Mganga Mkuu wa Mkoa, Bw. Eliakim Maswi kuhakikisha wanaanza na vitanda viwili hadi vitatu vinapatikana haraka ilikuwa na uwezo wa kusaidia wagonjwa wanaofikishwa hapo ilikupatiwa uangalizi maalum.
Dkt. Kigwangalla amebainisha kuwa, Hospitali kubwa kama hiyo kukosa chumba cha ICU ni hatari endapo itatokea tatizo kubwa hivyo kuagiza kulichukulia hatua za haraka.
Aidha, Naibu Waziri amesikitishwa na hali aliyokutana nayo kwenye maabara ya Hospitaali hiyo kutokuwa na damu za kutosha kwenye benki yake na kumuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Ally Uledi, kuanisha mipango ya upatikani wa damu salama katika kipindi cha siku 30.
Katika benki hiyo ya damu, Dkt. Kigwangalla aliweza kushuhudia kukiwa na damu unit 3 badala ya 150 zinazohitajika.
Aidha, Dkt. Kigwangalla alifunga safari hadi Wilaya ya Babati na kukagua kituo cha Afya Magugu na kukagua mambo mbalimbali katika kituo hicho huku akitoa maagizo ya kiutendaji huku akitaka apatiwe taarifa ambazo wanahitaji kusaidiwa zile zinazoihusu Wizara yake ilikushughulikiwa haraka.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akitoa maelezo kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Bw. Eliakim Maswi juu ya kufanyia marekebisho vifaa vya Maabara.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt.Hamisi Andrea Kigwangalla akiangaliaa benki ya damu ambayo haina kabisa damu licha ya kutolewa miongozo ya kila Hospitali kuwa na benki yake ya damu
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla (katikati) akipatiwa maelezo ya kutoka kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Manyara. Kulia kwake ni Mganga Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Ally Uledi,

..Ziara ikiendelea
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akitoa maelezo namna ya ramani ya chumba cha upasuaji kinavyotakiwa kujengwa
Chumba cha kutakasia vifaa maalum vya upasuaji
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akitafakari jambo wakati alipokagua chumba cha upasuaji.
..Wakisikiliza maswali ya watendaji wa Hospitaali
Baadhi ya viongozi na madaktari wa Hospitaali ya Mkoa wa Manyara wakifuatilia mkutano huo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akitoa maelezo kwa uongozi wa Hospitali ya Mkoa wa Manyara..
Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Bw. Eliakim Maswi akifafanua jambo katika mkutano huo.
ZIARA YA KITUO CHA AFYA MAGUGU WILAYA YA BABATI
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akiwasili katika Kituo cha Afya cha Magugu Wilayani Babati
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akisalimiana na watumishi wa kituo cha Afya cha Magugu Wilayani Babati
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akipata taarifa fupi katika Kituo cha Afya cha Magugu Wilayani Babati
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akipata maelezo katika chumba cha dawa katika Kituo cha Afya cha Magugu Wilayani Babati
Ukaguzi ukiendelea..
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akitoka katika jengo la Kliniki ya Afya ya Uzazi katika Kituo cha Afya cha Magugu Wilayani Babati
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akisaini kitabu cha wageni katika kituo cha Afya cha Magugu Wilayani Babati
Baadhi ya wafanyakazi wa Kituo cha Afya cha Magugu Wilayani Babati wakifuatilia mkutano maalum na Naibu Waziri wa Afya Dk. kigwangalla
Afisa Tawala wa Mkoa wa Mara akitoa maelezo machache ya kumshukuru Naibu Waziri wa Afya Dk. Hamisi Kigwangalla
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akitoa maelezo kwa viongozi na watendaji wa Kituo cha Afya Magugu Wilayani Babati wakati. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).
No comments:
Post a Comment