Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi akitia sahihi kwa niaba ya Serikali, Makubaliano ya Paris kuhusu mabadilio ya tabia nchi. Nchi 175 zimetia katika siku ya kwanza ya ufunguzi wa utiaji sahihi makubaliano hayo idadi ambayo imeelezwa haijawahi kutokea katika utiaji sahihi wa Mikataba au Makubaliano ya Kimataifa. Ili Makubaliano hayo yaweze kutekelezwa patatakiwa nchi 55 ziridhie na nchi hizo kwa ujumla wake ziwe zinatoa hewa ukaa kwa asilimia 55.
Hivi ndivyo ulivyokuwa Ukumbu Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Baada ya Katibu Mkuu Ban Ki Moon kutangaza kuanza kutiwa sahihi kwa Makubaliano ya Paris ambayo yalikubaliwa na nchi wanachama mwezi Desemba 2015.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe waliozungumza kabla ya utiaji sahihi wa Makubaliano ya Paris kutoka kushoto ni Hindou Oumarou Ibrah(Chad) aliwasilisha ujumbe wa asasi za kiraia, Bw Leonardo Di Caprio mcheza senema maarufu na Mjumbe Maalum kuhusu amani , na Getrude Clement ( Tanzania) aliyezungumza kwa niaba ya vijana
Na Mwandishi Maalum, New York
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni miongoni mwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa 175 ambao wametia sahihi kuhusu Makubaliano ya Mabadiliko ya Tabia nchi ( Paris Agreement) yaliyofikiwa katika mkutano uliofanyika Jijini Paris- Ufaransa mwezi Desemba 2015.
Balozi Tuvako Manongi, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa ndiyo aliyepewa dhamana ya kutia sahihi makubaliano hayo kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika hafla ya kihistoria na ya aina yake iliyofanyika siku ya Ijumaa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amesema haijawahi kutokea Mkataba au Makubaliano ya Kimataifa kutiwa sahihi na mataifa mengi katika siku ya kwanza kama ilivyokuwa kwa Makubaliano ya Paris.
Mataifa makubwa na ambayo yanachangia katika utoaji wa gesi chafu ya ukaa( carbon dioxide) kama Marekani, China, Urusi, India , Ufaranza na mengineyo nayo yameweka sahihi zao.
Aidha, Getrude Clement(16) kutoka Mwanza -Tanzania alizungumza katika hafla hiyo akiwakilisha ujumbe kutoka kwa vijana wenzie duniani kote.
Getrude alizungumza kwa umahiri wa hali ya juu, akianisha mambo kadha wa kadhaa ambayo vijana wa kizazi chake na kijacho wangependa kuona kizazi cha sasa kikiyatekeleza kupitia Makubaliano hayo ya Paris ili nao waje kuishi na kuifaidi Sayari Dunia.
“Mabibi na Mabwana sasa nina mkaribisha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa azungumze nanyi. Katibu Mkuu Karibu” akasema Getrude kauli iliyoufanya ukumbu mzima kumpigia makofi
Akizungumza baada ya kutia sahihi, Balozi Tuvako Manongi, pamoja na mambo mengine amesema, kwa Tanzania kutua sahihi Makubaliano nayo ni hatua moja kwenda hatua ya pili ya kuridhia.
Akasema, Tanzania inaserikali makini na Bunge makini ambalo kwayo limeweka mbele na kutilia mkazo suala la utunzaji wa mazingira na kwa sababu hiyo hapana shaka haitachukua muda mrefu wa kuridhia Makubaliaano hayo.
KUSOMA ZAID BOFYA HAPA.
STATEMENT PARIS AGREEMENT SIGNING CEREMONY
Mr President,
The Adoption of the Paris Agreement under the United Nations Framework Convention on Climate Change (UNFCCC) last December was truly historical. It was an important first step. It made possible the second step we are witnessing in the signing ceremony today. The proof of our resolve and commitment to making it all a reality hinges on the third step yet to be fulfilled; ratification and implementation of the Agreement.
The United Republic of Tanzania was among the first countries that submitted their Intended Nationally Determined Contributions (INDCs) on both adaptation and mitigation. It was a demonstration of our strong commitment to fulfil our obligations under the Convention and the Paris Agreement.
As a country, Tanzania is conscious that our fate and prosperity are inextricably linked to the effects of climate change. This is the essence of our INDCs on our adaptation and mitigation strategies. We will take a climate resilient development pathway intended to address climate related disasters and significantly reduce the impacts of climate change to our productive sectors and ecosystems.
We recognize the need to ensure economic growth that is sustainable, and less emitting in keeping with our National Vision to become a middle-income country by 2025. We have therefore focused our mitigation contributions on the following areas:
Forestry Sector
With 48.1 million ha of woodland and forests, of which 28 million ha (33 per cent) are under legal protection, Tanzania has a carbon stock of over 9 trillion tonnes and sequesters over 76 million tones of carbon dioxide despite emitting less than 50 million tonnes annually: It is a remarkable contribution we are committed to sustain and increase.
Energy Sector
We have resolved to make significant investments in natural gas to facilitate fuel switching by various end users to energy sources that are readily available and less emitting. To date, we are using over 140 million standard cubic feet of natural gas per day to produce over 690 MW of electricity. This contributes more than 2.2 million tones annually towards the global efforts to address climate change.
In addition, with over 57 trillion cubic feet already discovered, we hold considerable natural gas reserves whose future exploitation require financial and technological support and will contribute to further carbon reduction.
While we acknowledge the reality of climate change, we are mindful that the question of equity is crucial. Climate change affects us all, but it does not affect us all equally. Those who are least able to cope are most affected due to limited financial, technological as well as institutional and infrastructural capacities.
Those who have done the least to cause the problem bear the most severe consequences. In this regard, we are duty bound to right off this unfairness, and protect the most vulnerable. The Agreement we have signed today has made clear provisions for this consideration and deserves to be respected in full.
In Tanzania we have a national consensus and the necessary political will. We will seek and invite cooperation and partnerships. We will strive to access, acquire and deploy appropriate technologies for adaptation and mitigation in furtherance of a climate resilient, low carbon emission growth.
Finally, following our signature today we will begin our ratification process. We have a Government and a Parliament that is keen to see our Country playing its vital role in adapting to the negative impact of climate change and participating effectively in the global mitigation efforts.
I thank you.
" Mabibi na Mabwana sasa namkaribisha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuzungumza nanyi" ilikuwa ni kauli iliyowafanya wajumbe wa hafla hiyo kushangilia na kumpigia makofi, Mwakilishi wa Vijana, Getrude Clement (16) kutoka Mwanza Tanzania, mtangazaji wa radio, mwanaharakati kuhusu mazingira kwa kushirikiana na UNICEF. Aliyepewa fursa ya kuzungumza mwanzoni kabla ya kuanza kwa zoezi la utiaji sahihi.
Getrude Clement akiwa na ujumba wa Tanzania uliongozwa na Balozi Tuvako Manongi wakati wa utiaji sahihi wa Makubaliano ya Tabia nchi. ( Getrude) ni mwanaharakati wa mazingira kwa kushirikina na UNICEF.
Balozi Manongi akizungumza mara baada ya kutia sahihi makubaliano ya Paris kuhusu tabia nchi, ambapo alieleza kuhusu juhudi zinazofanywa na serikali katika utunzaji wa mazingira na matumizi ya nishati mbadala ambayo haitaongeza utoaji wa hewa ya ukaa. vile vile akasema Tanzania ina Serikali Makini na Bunge Makini na bila shaka mchakato wa kuridhia makubaliano hayo utaanza bila kuchelewa
No comments:
Post a Comment