Wednesday, May 4, 2016

Balozi Mkazi wa kwanza wa Tanzania nchini Kuwait awasilisha Hati za Utambulisho

Balozi wa Tanzania nchini Kuwait, Dkt. Mahadhi Juma Maalim (kushoto), akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mtukufu Shekh Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah (kushoto), Amir wa Serikali ya Kuwait katika sherehe zilizofanyika Ikulu ya nchi hiyo tarehe 03 Mei, 2016. Anayeshuhudia tukio hilo ni Makamu wa Kwanza wa Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Kuwait, Mtukufu Shekh Sabah Al-khaled Al-Sabah. Tanzania imefungua rasmi Ubalozi nchini humo mwaka 2015. 
Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim Balozi wa Kwanza Mkaazi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Kuwait, akiwasilisha Nakala za Hati zake za Utambulisho kwa Mtukufu Sheikh Sabah, Makamu wa Kwanza wa Waziri Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Serikali ya Kuwait kabla ya kuwasilisha Hati hizo kwa Amir wa Serikali ya Kuwait. 
Balozi Dkt. Mahadhi Juma Maalim (wa kwanza kushoto) akiwa kwenye mazungumzo na Mtukufu Shekh Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah (kushoto), Amir wa Serikali ya Kuwait mara baada ya kuwasilisha Hati zake za Utambulisho. 

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake