Friday, May 6, 2016

KESI YA KITILYA: MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI RUFAA YA DPP

Leo Mahakama Kuu Dar es Salaam imetupilia mbali rufaa ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashataka(DPP)dhidi ya Kitilya na wenzake, yaishauri Jamhuri kurudi Kisutu kufanya marekebisho ya shtaka hilo.
Jumanne wiki hii Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilisema kuwa jalada la kesi inayowakabili aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mwenyekiti wa Enterprise Growth Market Advisors Ltd (EGMA), Harry Msamire Kitilya na wenzake kimsingi bado lipo Mahakama Kuu na kwamba washtakiwa hao walitakiwa kwenda mbele ya Jaji Mfawidhi kwa maelekezo mengine.
Hayo yalisemwa na Hakimu Mkazi, Emilius Mchauru pale kesi ya washtakiwa hao ilipokuja kwa ajili ya kutajwa baada ya mawakili wa pande zote mbili kusema ya kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kupata maelekezo kutoka Mahakama Kuu kama ilivyoamuliwa mara ya mwisho.

1 comment:

  1. Ifike mahali tuwatambue mawakili wa Serikali wenye rekodi ya kushindwa kesi,ili tuwatumbue...

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake