Wednesday, May 4, 2016

MKUTANO KUHUSU MASUALA YA KIBINADAMU UWE WA VITENDO-TANZANIA

Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi akiwa na Mwakilishi wa Kudumu wa Denmark Balozi Ib Petersen wa kwanza kushoto ambaye waliiongoza pamoja mkutano usio rasmi ulioandaliwa na Mfuko wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa. Wengine katika picha Bi. Izumi Nakamitsu (UNDP) Bw. Mitiku Kassa ( Ethiopia) na Bi. Ahuna Eziakonwa ( UNDP)
Sehemu ya washiriki wa mkutano ulioandaliwa na UNDP ambao ulijadili kuhusu uzibaji wa tofauti kati ya mahitaji ya misaada ya kibinadamu na mahitaji ya maendeleo na namna gani nchi kwa kushirikiana na taasisi za umoja wa mataifa na wadau wengine wa maendeleo wanavyoweza kushirikiana katika kuyakabili majanga mbalimbali ya kibinadamu.
Sehemu ya washiriki wa mkutano ulioandaliwa na UNDP ambao ulijadili kuhusu uzibaji wa tofauti kati ya mahitaji ya misaada ya kibinadamu na mahitaji ya maendeleo na namna gani nchi kwa kushirikiana na taasisi za umoja wa mataifa na wadau wengine wa maendeleo wanavyoweza kushirikiana katika kuyakabili majanga mbalimbali ya kibinadamu.

Na Mwandishi Maalum


Wakati Jumuiya ya Kimataifa ikielekea kukamilisha maandalizi ya Mkutano Maalum wa Kimataifa kuhusu Masuala ya Kibinadamu, ( World Humanitarian Summit) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa upande wake, imesema , ni matarajio yake kwamba mkutano huo unatatoka na makubaliano yanayotekelezeka.

Kauli hiyo imetolewa siku ya Jumanne , na Balozi Tuvako Manongi, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, wakati yeye na Mwakilishi wa Kudumu wa Denmark Balozi Ib Petersen , walipoongoza majadiliano yasiyo rasimi kuhusu uzibaji wa mgawanyiko kati ya mahitaji ya kibinadamu na maendeleo; kutoka nadharia kwenda kwenye vitendo. Mkutano huo uliandaliwa Mfuko wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa ( UNDP).

“Mkutano ujao ni fursa nyingine kwa Jumuiya ya Kimataifa ya kuonyesha utashi wa kisiasa, kujadili kwa kina na tija changamoto zinazohusu ubinadamu na misaada ya kibindamu, ni fursa inayotakiwa kutumiwa vema katika utoaji wa ahadi na utekelezaji wa ahadi hizo kwa vitenda pasipo kumwacha yeyote nyuma”. Akasema Balozi Manongi.

Na kuongeza kuwa ingawa Tanzania kama nchi ambayo kwa maiaka mingi imekuwa ikiwapokea, kuwahifadhi na kutoa misaada ya kibinadamu kwa wakimbizi kutona nchi jirani, inautizama mkutano huo wa Instambul katika sura mbili tofauti.

Akasema moja ya sababu ambayo Tanzania inautizama kwa sura tofauti mkutano huo wa Instambuli kwamba umuhimu unaopewa mkutano huo, unakizana na umuhimu ambapo nchi kama Tanzania na nyingine hazikupewa au hazipwewi pale zinapokabiliwa na changamoto kubwa ya kuwawapokea na kuwahifadhi wakimbizi kutoka nchi jirani.

“ Tanzania tumekuwa kwa miaka mingi tukihifadhi wakimbizi, na katika miaka ya 90 tulipata changamoto kubwa sana ya kuwapokea na kuwahifadhi wakimbizi kutoka nchi jirani, matarijio yalikuwa ni kuona mwitikio wa haraka lakini haikuwa hivyo. Ushirikiano tulioupata ulikuwa wa kutoka Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa na Nchi za Scandinavia”. Akasema Balozi.

Mkutano wa masuala ya kibinadamu umeitishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon, utafanyika kati ya 23 na 24 mwezi huu wa March huko Instambul –Uturiki na unatarajiwa kuhudhuriwa na Viongozi wakuu wa nchi na Serikali, Taasisi na Mashirika ya Kimataifa yahusikayo na misaada ya kibinadamu .

Ni mkutano unaofanyika katika kipindi ambacho pamekuwapo na wimbi kubwa la maelfu ya wakimbizi wanaokimbia machafuko na vita katika nchi zao na kukimbilia nchi za Ulaya kutafuta hifadhi. Huku mamilioni wengine wakiwa ni wakimbizi wa ndani au wamekimbilia nchi jirani.



Balozi Manongi,Akabinisha pia kwamba hata katika Taarifa ya Katibu Mkuu inaonyesha kuwa bado kuna mapengo katika kughughulikia utoaji wa misaada ya kibinadamu, mapengo ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi kwa kuanzia kwa watoaji wa misaada, wasambazaji wa misaada hiyo hadi kwa walengwa wa misaaada hiyo. Na Akasisitiza Mkutano huo wa Instambul utatoa nafasi ya kujitizama upya na angalau kujafa jambo litakalo weza kuchangia kubadili hali ya sasa.

Mwakilishi huyo wa Tanzania, amewaeleza washiriki wa mkutano huo, licha ya kufanyika kwa mkutano mbalimbali ya kimataifa ukiwamo wa 2012 kujadili majanga ya kibinadamu, bado majanga hayo yanaendelea kuwapo huku ongezeko la hitajio la misaada ya kibinadamu likiendelea kuongezeka.

Akaeleza kwamba si kweli kuwa hakuna watu au wadau wenye mapenzi mema na wanaotaka kusaidia. Bali kinachotakiwa ni namna gani nchi zinazopata matatizo zinashirikianaje na kwa pamoja na Umoja wa Mataifa, na wadau mbambali katika kuyakabili matatizo hayo.

Balozi Manongi amebainisha pia kwamba Tanzania ingepeda kuona mkutano huo unatoka na mapendekezo yenye tija ya namna ya kumaliza migogoro na vita na ulinzi wa binadamu kwa kile alichosema asilimia 80 ya masuala ya kibinadamu na ubinadamu chanzo chake ni migogoro na vita.

Katika mkutano huo ambao Balozi Manongi na Balozi Petersen waliongoza nchi za Ethiopia, Pakistani na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo zilielezea uzoefu wao na changamoto katika kuyakabili majanga ya kibinadamu yakiwamo yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi, ukame na mafuriko, vita na machafuko na uhifadhi wa wakimbizi kutoka nchi jirani.

Nchi hizo zilieleza namna serikali kama zenyewe na kwa ubia na mashirika ya kimataifa na wadau wa maendeleo pamoja na wananchi walengwa ambavyo kwa umoja wao wameweza kutekeleza sera na mipango ya kujiandaa kwa maafaa kabla ya hayajatokea, namna zinavyo kabiliana na maafaa hayo yakisha tokea na baada ya kutokea.


No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake