Sunday, May 22, 2016

MUFTI WA TANZANIA ALAANI KITENDO CHA MAUAJI YALIYOTOKEA MKOANI MWANZA.

Shekhe Mkuu wa Tanzania ambaye pia ni Mufti wa Tanzania, Aboubakar Zubeir akizunumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, na kulaani kitendo cha mauaji ya watu wasio na hatia katika Msikiti huko Mkoani Mwanza. Kulia ni Msaidizi katika ofisi ya Mufti Mkuu wa Tanzania Shekhe, Ally Khamisi Ngeruko. na Kushoto ni Shekhe, Abuubakari Kharid.  Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

SHEKHE Mkuu wa Tanzania ambaye pia ni Mufti wa Tanzania, Aboubakar Zubeir pamoja amelaani vikali tukio la kinyama lililotokea Mei 17 mwaka huu katika Msikiti wa Ibanda Mkolani, Masjid Rahmaan mkoani Mwanza. 
Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo amesema kuwa kitendo hicho kuwa ni cha kinyama na hakivumiliki.

Tukio hilo lilitokea May 17 mwaka huu na kusababisha mauaji ya waumini watatu wa Msikiti wa Ibanda Mkolani waliokuwa katika Ibada miongoni mwao akiwa ni Imam wa Msikiti huo ikiwa na wengine kujeruhiwa.
"Kwaniaba ya Baraza kuu la Waislam wa Tanzania(Bakwata) tunalaani vikali tukio hili pamoja na kuwataka Waislam wawe watulivu katika kipindi hiki kigumu" Amesema Shekhe Zuberi.

Amewaomba Waislam na wananchi kwa ujumla kuvipa ushirikiano wa hali na mali vyombo vya usalam ili hatimae kuwapata waharifu hao ili waweze kufikishwa katika vyombo vya Sheria.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake