Dar es Salaam. Shule ya Sekondari ya Dar es Salaam, inayomilikiwa na Taasisi za Kiislam, Ilala jijini Dar es Salaam, imeteketea baada ya kuungua moto usiku wa kuamkia leo.
Shule hiyo ya Wasichana iliyoko pembeni mwa msikiti wa Taqwa, Ilala Bungoni, iliteketea jana majira ya saa tatu kasoro dakika kadhaa, kwa moto ulioibuka ghafla na kusamba kwa kasi ambayo baadhi ya viongozi hao waielezea kuwa ilikuwa ni ya kasi ya ajabu.
Katika tukio hilo, vyumba vyote vya madarasa na vya kulala wanafunzi hao pamoja na mali na vifaa mbalimbali vya shule na vya wanafunzi hao viliteketea vyote.
Ajali hiyo ilitokea wakati wanafunzi hao wakiwa katika maandalizi ya kufanya mtihani wa Mock. Hata hivyo hakuna mwanafunzi yeyote aliyepata madhara kutokana na moto huo kwani wakati ajali hiyo ikitokea wanafunzi walikuwa wakijisomea kwenye ukumbi nje ya madarasa na mabweni yaliyoungua.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Katibu wa Jumuiya za Kiislam (Jumiki) Sheikh Issa Ponda na mmoja wa Maimamu wa Misitiki ya Ilala, Othman Zubery, walisema kuwa moto ulioteketeza shule hiyo ulikuwa ni wa ajabu sana kiasi kwamba unatia mashaka kama ulikuwa ni moto wa kawaida, hasa kwa kuzingatia kuwa wakati tukio hilo linatokea hapakuwa na umeme shuleni hapo.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake