CHAMA cha Walimu (CWT) Rukwa, kimemkabidhi Mkuu wa Wilaya ya
Sumbawanga, Mathew Sedoyeka ushahidi wa maandishi unaoelezea kitendo cha
Ofisa Elimu, Shule za Msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya
Sumbawanga, Peter Fusi, kumshambulia na kumpiga makofi mwalimu mwenzao
akiwa darasani.
Ushahidi huo ulikabidhiwa kwa Mkuu wa wilaya na Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Rukwa, Hance Mwasajone.
Ushahidi huo wa kimaandishi wa tukio hilo umeandikwa na mwalimu
mwenyewe, Jacob Msengezi (25) ambaye alisema alipigwa mbele ya wanafunzi
wake akiwa darasani shule ya msingi Kianda kabla ya kuamuru walimu
wengine kufanya usafi kwa kuokota mbigili ‘miba’ iliyotapakaa katika
eneo la shule hiyo akidai kuwa huo ni uchafu.
Sedoyeka aliwaruhusu viongozi hao kumtembelea mwalimu na kusisitiza
kuwa anafuatilia kwa karibu mkasa huo ili sheria ichukue mkondo wake .
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake