Mwenyekiti wa Bodi ya UTT-PID, Bi. Elpina Mlaki akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mh. Godfrey Zambi wakati wa mkutano huo ambao jumla ya Bilioni 2, za mradi wa viwanja kwa Manispaa ya Lindi ziliweza kupatikana katika mradi wa upimaji viwanja.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi (katikati) akizungumza na wajumbe wa mkutano huo uliojumuisha uongozi wa Mkoa wa Lindi pamoja na Bodi ya UTT-PID ikiambatana na Menejimenti yake.
.
Akielezza Mkurugenzi wa Manispaa hiyo ya Lindi, Bw. Jomaary Satura wakati wa kikao cha kuangalia mafanikio kilichofanyika jana, ambapo alibainisha kuwa, fedha hizo ni mafanikio ya upimaji wa viwanja 2,500 kati ya 10,000 walivyokusudia kupima awamu ya kwanza.
“Fedha hizi zimetumika kujenga miradi mbalimbali kwenye Manispaa yetu. Ikiwemo kujenga Maabara na vifaa vyake, Ujenzi wa Zahanati, Nyumba ya Mganga na Boti ya kisasa.” Alieleza Mkurugenzi huyo.
Aidha aliongeza kuwa, mapato ya ndani ya ndani kwa sasa yameongezeka kwa kupanda kutoka Sh 700 Milioni mwaka 2013 hadi Sh 2.4 Bilioni.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya UTT-PID, Bi. Janet Mmari amesema mradi huo umegharimu Sh.1.9 Bilioni hivyo umeonyesha mafaniko kwa jamii.
“Mradi huu ulikuwa ni wa gawio la asilimia 50 kwa 50. Tunawapongeza Manispaa kwa kufanya kazi vizuri” alisema Bi. Janet Mmari.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi alisema kuwa, awamu ya pili watashirikisha makundi yote ikiwemo wanasiasa ilikuondoa mivutano inayosababisha kuchelewa kwa maendeleo.
“Maendeleo yanapatikana mawazo yanapogangana. Nyingine ni changamoto za kawaida na uelewa, Wanasiasa kuingilia kunatokana na masilahi binafsi” alieleza Mkuu wa Mkoa huyo.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake