Saturday, May 21, 2016

WACHAGA WAKUMBUSHWA KUISAPOTI TIMU YAO YA KILIMANJARO INAYOSHIRIKI LIGI YA MABINGWA WA MIKOA.

Mwenyekiti wa Chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro,(KRFA) Godluck Mosha akizungumza wakati wa kuwaaga mabingwa wa soka mkoa wa Kilimanjaro, timu ya Kitayosce wanaojiandaa kuelekea mkoani Singida kushiriki ligi ya Mabingwa wa mikoa katika kituo hicho.
Baadhi ya wachezaji timu ya Kitayosce wakiwa katika uwanja wa Meimoria ambako waliagwa na uongozi wa Chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro (KRFA)

Katibu wa Chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro (KRFA) Mohamed Musa akizungumza wakati wa kuiga timu ya Kitaysce.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya Kitayosce.
Mjumbe wa kamati ya kuisadia timu ya Kitayosce,Dalabu Maulid Dalabu akizungumza katika hafla hiyo fupi.
Mwenyekiti wa Chama cha soka Manispaa ya Moshi (MMFA) Japhet Mpande akitoa nasaha zake kwa wacheaji wa timu ya Kitayosce wakati wa kuiaga timu hiyo.
Kocha wa timu ya Kitayosce,Hamad Haule akielezea matarajio yao katika ligi ya mabingwa ambapo timu yake imepangwa kituo cha Singida.
Nahodha wa timu ya soka ya Kitaysce ,Chimko Vidic akieleza namna walivyojiandaa na ligi hiyo.
Mwenyekiti wa Chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro (KRFA) Godluck Mosha akimkabidhi Mweka hazina wa timu ya Kitaysce ,Festus nauli kwa ajili ya safari ya kuelekea Singida ,KRFA imetoa nauli ya kwenda Sindida na kurudi.
Mwenyekiti wa Chama cha soka Mkoa wa Kilimanjaro,(KRFA) Godluck Mosha akikabidhi mpira kwa ajili ya timu ya Kitayosce.
Mwenyekiti Mosha akikabidhi kiasi cha Sh Laki moja kwa nahodha wa timu ya Kitayosce kwa ajili ya kunua viatu kwa baadhi ya wachezaji wa timu hiyo.
Wachezaji wa Kitayosce wakiagana na Viongozi wa KRFA katika uwanja wa Meimoria. 

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
Mabingwa wa soka mkoa wa Kilimanjaro,Timu ya Kitayosce inataraji kuondoka jumapili hii kuelekea Singida huku ikikabiliwa na ukata .

Kamati ya kuisadia timu hiyo imeendelea kuhamasisha wadau mbalimbali wa soka hasa wale ambao ni wenyeji wa mkoa wa Kilimanjaro kujitokeza kuisadia timu hiyo kwa hali na mali ili iweze kuuwakilisha vyema mkoa wa Kilimanjaro.

Hata hivyo kamati inatoa pongezi kwa Kampuni inayosimamia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro KIA(KADCO) kwa msaada wa awali iliyotoa huku ikiwakumbusha wadau wengine waliofikishiwa barua za ombi la msaada kwa timu hiyo kuzifanyia kazi.

Kwa sasa kamati ya kuisadia timu hiyo inakusanya michango kupitia namba za simu 0715331274 na 0746331274.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake