Wednesday, May 18, 2016

Wosia wa Le Mutuz kwa Wanaowaza Kwenda Kuishi nje ya Nchi..


Leo i want to touch this very sensitive subject ya wanaodai kuwa inapokuja kwenye diaspora huenda nina wivu na chuki na wanaoishi majuu kwa sababu nilirudi, ha! ha! ha! kwa wale ambao hamjafika majuu naomba kusema hivi:-
 mungu alinijalia sana confidence in myself na everything i do, nilipofika majuu kwa mara ya kwanza nilikuta wabongo karibu wote pale New York wanafanya kazi za kulinda na kutunza wazee na mataharia, siku moja mbongo mmoja alinipeleka kwenye kazi ya kutunza mataahira nilikaa kama lisaa limoja tu sikurudi tena, nikaenda shule kutafuta leseni ya cdl ya kuendesha malori makubwa sana ambayo hapa bongo hayapo, kazi ambayo inalipa haswa nikahangaika mpaka nikapata ile leseni nikiwa ninafanya kazi gas station mchana na usiku Kentucky Fried Chicken. Nilipopata leseni nikaanza kuendesha malori America nzima. Wale wabongo niliowakatalia zile kazi zao wakaanza kunizushia maneno kwamba ninauza unga, ha! ha! ha! ha!,

Kabla ya kwenda New York nilishakuwa baharia Belgium so Ulaya haikuwa kitu kigeni kwangu, ndio maana siku moja nikaamua kurudi Bongo mwenyewe bila kulazimishwa na mtu. Cha kwanza nilipofika tu bongo nikaanza kunenepa, why? Kwa sababu ni kwa mara ya kwanza katika miaka 30 ya maisha yangu nimeweza ku-relax na maisha. Majuu ni kufanya kazi tu na kulipia madeni, wazungu sio wajinga wameitengeneza system yao to the point wewe unaenda kuchangia uchumi wao tu hauwezi kuwa tajiri maana uwezekano haupo, wewe ni kazi tu, social life hamna ni kazi tu kila ukikaa unawaza kazi, mabebez hamna, wachache wabongo waliopo ni hasara tupu wengi wao hawajitambui. Kwenye uzungu hawapo kwenye ubongo hawapo wapowapo tu ole wako uwaguse, i mean kila kitu majuu ni perfect lakini gharama yake haikupi nafasi wewe kuwa na pesa extra, ndio unagundua kwamba majuu sio kama ulivyotegemea maisha ni mazuri lakini magumu sana kurudi bongo nako huwezi maana ni noma zaidi so you are stuck, i was stuck too mpaka nilipoamua kwa hiari yangu kurudi home.

Hapa sina deni kwa mara ya kwanza katika maisha yangu, sidaiwi na mtu kila nilichonacho, kama ni gari ni langu, apartment ni yangu, shamba na nyumba ni vyangu sidaiwi na mtu, nafanya kazi ya kujiajiri, nakuja kazini saa ninayotaka, ninatoka saa ninayotaka, kwa mara ya kwanza ninamiliki simu za usd $ 1000 a piece majuu ningekuwa nayo ya kukopa na sikuwahi kuwanazo, bongo maisha baada ya kazi hayana mfano, marafiki kila kona kule unakuwa huna marafiki, bongo heshima kila kona majuu mweusi atakuheshimu nani? i mean kwenye kujiajiri nikipiga deal moja ikaitika millions zinakuwa zangu sio kulipia madeni, ninasafiri bongo na nje ya bongo anytime i want majuu nisingeweza maana ni kazi tu all the times.

Sasa naomba kuuliza jamani kweli niwaonee wivu na chuki waliobaki majuu kwa kisa gani? nasema hivi majuu wanatuzidi bongo kwa one thing matibabu wao wakiumwa kule ni rahisi sana kupona kuliko hizi hospitali zetu bongo, ni hilo tu mengine hapana bongo kuna maisha asikudanganye mtu, again mungu alinijalia moyo wa kujali yangu zaidi na sio ya wengine so kwa wale mnaolia lia kwamba nawaonea wivu eti mko majuu ha! ha! ha! ha! please!!, ninafanya biashara na wabongo wengi huko nje inapokuja kwenye kulipa ni kivumbi na patashika lakini hapa bongo ni tofauti watu wanalipa mara moja tena mpaka kwa dola za kimarekani, jamani kwa wale ambao hamjafika huko majuu na unaweza kula milo mitatu bongo bila tatizo tulieni hapa hapa jamani huko majuu kusikieni tu!!, ninamshukuru mungu kila siku kwa kunipa akili ya kwenda majuu na pia ya kurudi home ontime kabla sijachelewa, ndugu zangu huko rudini huku bongo maisha ni sawa ila tu ujipange kabla ya kuja na muhimu kuliko yote soma shule kwanza, huku bongo bila elimu utachekesha maana hela ukijanazo zitaisha kama huna elimu. jamani samahani kwa maelezo marefu lakini i hope nimemsaidia somebody out there!! - Le mutuz.

30 comments:

  1. Ulichosema mzee ni kweli kabisa

    ReplyDelete
  2. (1) Mr man, life principles are the same everywhere

    (2) Never you make general assumptions to suit your situation or opinion at a moment. There are highly qualified individuals in the diaspora that have descent highly paying professional careers in fields such as Computer Sciences/Engineering,Pharmacy,Medicine, Business etc.


    (3) Not everyone who lives abroad is in debt, that is not true

    (4) Not everyone is carrying boxes and work non stop with no time for themselves or their families, that is not true! There are people here who works descent hours, under very conducive and respectful
    working environment with great benefits, saving plans and great retirement programs

    (3)There is a lot of successful entrepreneurs who are running very successful businesses and they are from Tanzania to be very specific

    (4)Those who just go abroad and are not paying attention to true principles of hard work, best education, networking,honesty, perseverance , determination will not be successful. But this is true to those that are not abroad also

    (5)You have said some truths in your article and that is home is home, home is always the best

    (6)Remember life principles are the same ukiwa Tanzania au ukiwa nchi yoyote ile duniani



    AMANI




    ReplyDelete
  3. .mtoa mada huna nyimbo..na yamekushinda mengi. Tunakustahi tuu..
    Vilevile kunamsemo usemao "UZURI WA JAMBO UULIZWE"...sasa wewe umeulizwa?..acha kimbelembele

    ReplyDelete
  4. natae mm umeongea vizuri sana. kama mtu hatakuelewa, basi kaamua kutokukuelewa. Sijui kwa nini watu wanapenda kuegemea tuu upande mmoja? Mnaangalia tu wanaohenya, mbona hamuangalii wanaofanya vizuri kimaisha? Soo sad.

    ReplyDelete
  5. U have said the truth my dear,, hata mimi ningejuwa nisingekuja huku ni kweli wapinge wacheke make money or not make money ni bure huku tuko jera ya kaz tuuu big up wambien wajue kabla waje huku kuliko waje kulia nakusumbuwa watu,

    ReplyDelete
  6. Sasa huyo lemutuz kwanini hakuingia shule alivyokuja kwanza..probably angepata kazi ya maana na sio kuendesha malorry...ni wenyeji wako waliokukaribisha wange kuonyesha the right path...

    ReplyDelete
  7. Nipo America for 17 years now. Anachokisema Le Mutuz ni kweli tupu pamoja na kwamba wapo wachache hapa America ambao wako sawa kiamaisha ila wengi wetu tuko hoi.
    Bila ya kuwa bias nasema Ahsante sana kaka kwa ujasiri wako na kusema ukweli mtupu.

    ReplyDelete
  8. Mbona hujasema kama ulikimbizwa na child support??( matunzo ya watoto) uliokuwa unadaiwa? Hukuondoka kwa hiari yako. Kama ni kweli uliondoka kwa hiari yako njoo katembee Marekani basi. Acha upuuzi!

    ReplyDelete
  9. This old man let his mouth go ahead of his brain, he is a loser and I have seen many loser like in my life. He doesn't know that he also has responsibility to his uninformed audience. Total waste!

    ReplyDelete
  10. Acha upimbi wewe le mutuz,siumekimbia child support.you abondened your kids man.Watu wapo huku tuna invest bongo nunua viwanja sehemu poa kigamboni, tegeta,pugu,jenga apartments unapangisha watu.mchuzi huko huku wewe kujutana tu.BONGO kazi kupata shida.Usiwachuze watu UNYAMWEZINI babukubwa.

    ReplyDelete
  11. Tatizo lako wewe lemutuz inaonekana hauna upeo wa kutosha kuhusu watu wanaoishi usa.
    Tatizo la huku Marekani, ukiwa kwenye circle yako haujui what is going on the other end. Wewe ulizungukwa na watu wanaolea wazee na mataahira kwa hiyo ukadhani kuwa kila mtu anafanya kazi hiyo, siyo kweli.

    Mara nyingi watu wanaofanya kazi hizo ni either, ndiyo wamekuja bado wapya, wanafunzi, wasio na makaratasi, au watu wazima ambao hawawezi kwenda shule, ni kazi rahisi sana kwa watu wazima na wengi wao wanaweza kutunza familia zao huko nyumbani n ahata kujenga kwa kazi hizi hizi. Vilevile watu ambao huwa wanafikia miji mikubwa (kama vile DC, NY, NJ) mara nyingi huwaga wanafanya hizi kazi kwa sababu either maisha yapo juu sana au wenyeji wao hawawaonyeshi njia nzuri ya kwenda. Watu waliofikia kwenye miji migodo, almost wote wamekwenda shula and most of them wana professional jobs au biashara zao.

    Sasa, on the other side (ambaoyo wewe kwa bahati mbaya wewe haukuwepo), kuna watu professional, and fyi there are so many Tanzanians doing very professional jobs in the US, and some of them work for Government. Hawa watu wanafanya kuanzia 9am to 5pm, wanarudi home and spend time with their families (siyo kwenda bar). Hawa watu wana njia nyingi tu za kusave pesa, kama vile 401k, buying stocks, etc. I have hundreds and hundreds of Tanzania professional friends on LinkedIn….very professionals...some are working for the Homeland Security, Google, big financial firms, etc.

    Watu wengi wa USA hawataki kunenepa kwa sababu wanajua madhara yake, sasa kama wewe unadhani kunenepa ni kwa sababu ya ku relax, then good luck on that.

    Kuhusu madeni, it is normal kwa nchi za kibepari au zilizoendelea, hata ukienda South Africa an Kenya, mambo ya mortgage yapo long time, kwa hiyo hiyo ni system tu, why buying a car for $25000 cash while you can pay $150 monthly? Kwa hiyo unapotafuta kazi unajua kabisa kuwa kwenye mshahara utatoa $150 kila mwezi kwa malipo ya gari, so it is not a big deal.
    Watu wengi hawataki kurudi Tanzania kwa sababu wana familia huku, huwezi kumtoa mtoto wako USA aje kusoma Tanzania, kwa hiyo wanasubiri watoto wakue and then wanajikuta wameishaingia kwenye system, na ukishaingia kwenye system ya USA hautaweza kuishi bongo. Huku hakuna uonezi, rushwa, majambazi, maradhi, ajali za kijinga jinga, unyanyasaji, etc
    Kwa hiyo bhana, wewe Lemutus, inabidi ufanye research kwanza halafu uandike unachoandika. Kama kuna mtu anataka kwenda USA, especially vijana, nendeni tu, you just need to know what you are going there to do, and be a good citizen utafanikiwa tu. This is the only country where unakuja na nothing and you end up very successfully.
    Please don’t listen to this man 

    ReplyDelete
  12. Facts:

    First, this guy is not educated. If you go anywhere in the world with Le Mutuz's level of education and mentality, you will never succeed.

    Second, if what he says is true, then, why majuu are more successful than they so called third word countries (including Bongo)?

    Kama alifvosema mdau hapo juu "Life principles are the same everywhere". That should be a take home message.

    Finally, kubwa jinga is just a loser. End of story!

    ReplyDelete
  13. Nahisi ili li kaka ni jinga,ivi alijui maisha ni kuhangaika,yeye alikuwa dereva huku ,wengine sio madereva huku sasa hivi Kuna watanzania kibao huku maisha yao yapo ok,wa namiliki hayo malori,yeye alikuwa dereva huku ,kwa elimu yake alichojifunza huku ni freedom of speech wala sio zaidi ya ilo,ndio maana yupo bongo kwa kuishi kwa kujionyesha kwenye mitandao,ni mpumbavu kama yeye tu ndio mwenye tabia za kijinga kama yeye kuongea upumbavu huo,maIsha ni popote kaka,huku tupo tuna faida nyingi tu,elimu ya watoto ni mtaji,matibabu,hela yangu kwa wiki ninayotengeza huku ni mapato yako ya miezi miwili huko

    ReplyDelete
  14. Tatizo umeandika na jaziba kujipa moyo na muwapa moyo wale ambao wamekuwa deported au wamefanya wizi na matokeo yake kushindwa kukaa ughaibuni. Unawezaje kulinganisha 3rd world na mataifa ya ulaya? Afu unasema nani atakuheshimu mtu mweusi Ulaya. hivi bongo kuna wazungu? weusi wa bongo wanaheshimiana wao kwa wao tu? Vipi nje ya bongo, bado wanaheshimiwa? kwa nini?Kwa hiyo wewe ni advocate wa kutofanya kazi?

    ReplyDelete
  15. Fact check. Hivi kweli alitoka huko majuu kwa hiari? Mbona nilishasikia swala la kids support? Labda tuulize wanaofahamu zaidi. Ama mtu atuvutie records za Mahakama ya mji alipoishi.

    ReplyDelete
  16. Sio kweli kwamba Ulaya ni pabaya. Huwezi kulinganisha 3rd world country na Ulaya hata kama una hasira. Hivi ni vichekesho! Ndio Ulaya unafanya kazi. Kinachosababisha mataifa yetu ya africa yawe nyuma ni hicho, kwamba watu ni wavivu.
    Twambie basi unatumia muda gani barabarani from point A to B ukiwa Dar. Au ukitaka kuoga, maji yanatoka au kwanza uombe? Bill ya umeme inakuja bei gani ukiwasha ac (kama unayo). Chakula miro mitatu? Usinichekeshe. Hiyo sio bongo. Chakula ni cha shida sana ukizingatia uvivu wa watu. Ukienda hoteli nzuri wanakuuzia chips kavu kwa elfu 50. Wizi mwingi na kazi hamna. Karibu kila mtu mwizi. Customer care sio nzuri kabisa. Hotelini mhudumu anakuja na njiti mdomoni, tena anakufokea wewe mteja. Barabarani, hasa dar ni kama vita. Mwenye nguvu ndo anapita kwanza na gari. Huwezi kuwasha ac ndani ya gari na foleni zote. Hakuna ulinzi. Yaani unaweza kutembea kutoka Morocco hadi Tegeta hujakutana na polisi au kuona kituo cha polisi labda uwe kiongozi wa chadema tu, hapo polisi watakufata kila kona.
    Kwa hayo machache napenda kukwambia kwamba usijaribu kabisaa kulinganisha Ulaya na nchi zilizoendelea. Waliokupoteza ni wale walokupokea ila siwalaumu. Nakulaumu wewe mwenyewe. Bado ungeweza kufanya vizuri. Wengi wanaotoka Ulaya wanakuwa na issues kama za wizi mkubwa, child support, uhamiaji nk. Ni wachache sana wanaoamua kurudi nyumbani. Nadhani wewe umo kwenye hizo category.
    Siamini bongo unaweza kufanya biashara na mtu yeyote. Watu hawajui networking. Wengi wao ukimpa deal zuri tu, anasubili kukuibia, basi. Hii ndo sifa yetu internationally kwa sasa.

    Nikuulize swali la mwisho, kwani usingeweza kufanya biashara bongo ukiwa ughaibuni kama unavyosema kwamba unaingia ofisini unavyotaka? Mimi unaniaminisha kwamba hapo unaweza ukawa ughaibuni bado biashara ikaenda au kinachoshindikana ni nini kama mambo huko ni mazuri?

    ReplyDelete
  17. lemutuz is dead beat father ana watoto kawaacha marekani wala ata hawajali, yeye kutwa kujirusha na wakina diamond ambao ni kama wajukuu zake,dude is almost 60 yrs by still acting like teenager,kuna watu wanafanya kazi professional hawana haja ya kuutangazia umma na ata hao wanaofanya kazi hizo ulizozitaja wengi wamefanya mambo ya maana bongo na wanasomesha pia,na wanafanya kazi halali,sasa nyie na shughuli zenu za ujanja ujanja na kujuana usiache mbali na hela za ufisadi na sembe mnaanza kutukana watu?ndio maana mungu alimleta magufuli bongo ili awanyooshe kwa kipindi cha miaka kumi ijao.

    ReplyDelete
  18. Huyu Lemutu, mbona analalamika sana? Amshukuru Mungu kufika Amerika , naakajifunza mengi, maisha ni popote.
    Mbona wako waliotoka Urusi, ujerumani, China hawalalamiki kama huyu?
    Pole sana kaka, kuendesha malory ni dhambi kwani? Au nyumbani kwako hata vyombo huoshi, au kupiga nguo pasi? Kama ndio kazi halali haina haja ya kuidharau wako wenye masters na kazi hawana Mungu akufungue kaka asante.

    ReplyDelete
  19. Hivi siyo wewe uliyeondoka NY kwa sababu ya child support na mpaka leo unatafutwa na warrant yako uko bado? Wacha kudanganya watum ulirudi mwenyewe kwa history yako maana hii ni uongo mfupi. We kama ni mjanja na mwanaume wa ukweli anakimbiaje mtoto uliyemzaa? Wanaume hawakimbii majukumu yao tena watoto! Wengine tunakazi zetu za maana hatuangalii mataahira wala kuchunga wazee kwa hiyo usituweke kapuni. We kama umerudi endelea na maisha yako ya wengine yanakuhusu nini? Bwege kubwa jinga tu wewe.

    ReplyDelete
  20. Ukimuondoa David Mosha na few other fellows wanaomfadhili Katika equation ya the so called mafanikio ya Lemutuz bongo,huyu bwana hana kitu.

    ReplyDelete
  21. ulirudi mwenyewe au ulirudishwa? wenye pesa hawasemi! Maisha hata bongo ni magumu hivi umeona watu wanavyoshinda siku nzima bila chakula. Si ajabu ni majirani zako unawapita kila siku na unashindwa kuwasaidia. Uwe makini na mausia ya kujumlisha kila mtu. sio kila mtu anaishi maisha ya shida kama uliyoishi wewe au unayoishi sasa. Vidole vya mkono mmoja havilingani. Siku nyingine ukiwa na lakuongea jaribu kupata mausia na hekima sio unakurupuka. I think you could give people advise especially those who are struggling on how to improve their lives and not to look down on people and all over sudden you think you are above every one. hata wewe huku bongo husikiki.

    ReplyDelete
  22. Si mpingi kwa kitu chochotehila jamaa kawa na hasira Sana na watu wanao ishi marekan moja tangu hatoke huku Mada zake ni jinsi halivyo hishi maisha ya shida 1 yeye halikua mtoto wa na b i halivyo Kuja hapa kulinganisha na wengine waliotokea kwenye shida pili bado linashindwa kusema hukweli hayo maroli hanayo Sema Tanzania hayapo ni ya Aina gani kwani najua Gari halilokua hanaendesha halizidi hata Tani 20 vijijini yapo Tena mengi pili jamaa hanashindwa kuelezea matatizo yaliompata halijaza ma credit card na kutumia kijinga kushindwa kulipa haka kimbilia bankruptcy na bahati nzuri hakapata kwahiyo hizo stress sio kila mtu hanazo mi naona humeondoka just mind hulipo na watu hunao hishi nao make hapa mount Vernon hulikua humekalibia kuwa alone watu walisha kuogopa sababu ya kua kama shoga

    ReplyDelete
  23. Nimeishi America for 17 years. I have full experience with this life. Le mutuz anaongea ukweli mtupu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Dogo upo kwa OBAMA au kimanzichana....mtoto wa kiume ww kaza nwana unataka seleleko...watakudandia wajanja angalia

      Delete
    2. Inaelekea na wewe ni walex2..

      Delete
  24. Nacho kushauri kwamba, endapo wewe huku fainikisha kimaisha hapa States kwa sababu zako binafsi,haimaanishi wote wapo katika hali uliyopitia. Tupo tuliokuja hapa kimichezo na hatimaye kufanya kazi nyingi za bila degree wakati tunaenda chuoni na sasa tunaishi maisha ya kati bila hofu na mambo mengi kama uliyoongelea hapo. Bora niwe hapa na ujuzi niliopata College US, kuliko kuwa TZ ambako sintoweza kuwa na mapato kama nipatayo hapa.Kila la kheri na maisha yako ya Bongo!

    ReplyDelete
  25. ILI JAMAA NI KAMA KUBWA JINGA, NAFIKILI LIMEKUWA NA UMBO KUBWA KWA KULA VYA BURE, UMEKIMBIA WATOTO HUKU, MKEO WENZIO WANAFAIDI HUKU, WEWE UKIKANYAGA HUKU URUDI MAANA WANAKUTAFUTA UNAYO WARRANTY, UNAONEKANA UNANENEPA KWA KURA VYA BBURE HUKO, UNAISHI KWA MSAADA WA DAVIS MOSHA, MWENZIO ANAZITAFUTA , WEWE KAZI YAKE UPANDE, NAHISI LAZIMA UTAKUWA UNAUGUA KICHAA, MAISHA YA WATU WA MAMTONI YNAKUHUSU NINI WEWE SHOOGA LA MCHANA, ACHANA NA WATU WA VIWANJA BAKIA NA USHOGA WAKO HUKO

    ReplyDelete
  26. C'mon people relax!Everyone's entitled to their opinion.We can all agree to disagree.Maisha ni popote neema inapokushukia.Kwetu wengine ni hapa na wengine ni bongo au popote duniani.So long you are still breathing you can make it anywhere.Kitu kimoja atleast huyu kaka anaguts za kutoa opinion yake bila kujificha naona hapa bandugu wengi anonymous.Cheer up people life is too short!

    ReplyDelete
  27. Mmmh! Ungesoma shule lemutuz husingekuwa dereva na badala yake unge own hayo ma trucks bwana. Watu wamesoma na wana own business kibao. Acha tabia ya kuongea kwa sababu unabifu na kundi ka watu fulani unaunganisha watu wote. Dunia nzima kuna watu wanao struggle hata wamerekani wa kuzaliwa wapo ma homeless kibao..lkn wewe inaonekana una hasira na watanzania wanaoishi matekani. Mbona bongo sasa hivi magufuli ndio anaanza kuisafisha. Angalia na wewe husije kuwa jipu. Maana utatumbuliwa bongo hakuna pa kutorokea mmebanwa vizuri sana...lol! Big up magufuli...hilo nalo jipu...

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake