Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii katikati Maj. Gen. Gaudence Milanzi akita utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Onesho la Historia ya Chimbuko la Mwanadam lililopo Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni DSM. Wanao shuhudia kuliani Mwenyekiti wa Bodi ya Makumbusho ya Taifa Mh Anna Abdala na kushoto ni mwakilishi wa Balozi wa Spain nchini Bw Bw Guilaume M. Juarez , Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Prof Audax Mabula na Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dsm Bw Achiles Bufure.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Maj. Gen. Gaudence Milanzi na wageni wengine wakipata maelezo ya historia ya chimbuko la Mwanadamu kutoka kwa Maratibu wa Onesho hilo Dr Agnes Gidna.
Mwenyekiti wa Bodi ya Makumbusho ya Taifa Mh Anna Abdalla akilitazama moja ya fufu la Binadamu wa kale wanaosadikiwa waliishi takribani miaka Milioni 3.6 iliyopita.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Maj. Gen. Gaudence Milanzi na wageni wengine wakipata maelezo ya historia ya chimbuko la Mwanadamu kutoka kwa Maratibu wa Onesho hilo Dr Agnes Gidna.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Maj. Gen. Gaudence Milanzi na mwakilishi wa Balozi wa Spain nchini Bw Bw Guilaume M. Juarez wakiangalia kwa umakini mkubwa masalia ya wanyama wakale walioishi trakribani miaka Milioni 4 iliyopita.
Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii nchini Maj. Gen. Gaudence Milanzi amesisitiza
kuwa Tanzania ndio nchi pekee Duniani yenye ukweli wa kisayansi
unaothibitisha kuwa ndipo binadamu wa kwanza alipo patikana na kuanza
kusambaa maeneo mengine Duniani na si kama baadhi ya nchi zinavyo jitangazia
kuwa uridhi huu wa kihistoria ni wao.
Ameyasema haya kati ufunguzi wa Onesho kubwa la Kihistoria lililopo
Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni lenye kuonesha ukweli huu wa
kisayansi uliotokana na Tafiti mbali mbali zilizo fanywa na watafiti Duniani kama
ule wa Laetoli mwaka 1978 na mtafiti Dkt. Mary D. Leakey zinazo onesha nyayo
ziliachwa na zamadamu anayeiitwa Australopithecus afarensis na ni ushaidi
usiopingika wa zamadamu kutembea wima kwa miguu miwili takribani miaka milioni
3.6 iliyopia.
Akizungumza katika ufunguzi wa Onesho hilo kwaniaba ya Balozi wa Spain nchini
Msaidizi wa Balozi wa Spain nchini Bw Guilaume M. Juarez alisema kuwa
binadamu wote tunapaswa kuheshimiana kama ndugu kwani tafiti nyingi Duniani
zinadhihirisha ukweli usiopingika kuwa binadamu wote duniani wametoka Afrika na
ni Tanzania hivyo watu wote ni watanzania.
Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Prof Audax Mabula na Mwenyekiti wa
Bodi ya Shirika la Makumbusho ya Taifa Bi Anna Abdala, wametoa wito kwa
watanzania wote hususani waliopo jijini Dar es Salaam hasa wazazi na watoto
kuitembelea Makumbusho hiyo kwa lengo la kujifunza uwalisia wa ubinadamu wao
badala ya kutumia muda mwingi kwenye sehemu zingine za starehee.
Onesho hilo la Chimbuko la Mwanadamu lililopo Makumbusho na Nyumba ya
Utamaduni Dar es Salaam, Mtaa wa Shaban Robart mkabala na chuo cha
Usimamizi wa Fedha IFM sambamba na maonesho mengine litakuwa wazi kuazia
saa tatu asubuhi na kufungwa saa 12 jioni kila siku za Juma.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake