Advertisements

Friday, July 8, 2016

POLISI WANNE WAUWAWA KATIKA MAANDAMANO JIJINI DALLAS

Mdunguaji amewapiga risasi na kuwauwa polisi wanne na kujeruhi wengine saba huko Dallas, Marekani katika maandamano ya kupinga mauaji ya watu weusi yanayofanywa na polisi.

Milio ya risasi ilisikika wakati waandamanaji walipokuwa wakiandamana katika mji huo. Mtu mmoja anashikiliwa na polisi na mwingine mmoja aliyeonekana na bunduki amejisalimisha.
        Polisi wakiwa kazini wakimsaka mdunguaji 
Hali ilikuwa inatisha kiasi ya watu kujificha kwenye magari wakati polisi wakihaha kumsaka mdunguaji
Huyu aliamua kundamana na bunduki yake, na sasa amejisalimisha polisi kwa mahojiano zaidi.

2 comments:

Anonymous said...

Nilishahisi jambo kama hili litatokea, zile taarifa zilizokua zinaonyeshwa jana na juzi zinatia huzuni kisha kupandisha hasira kwa wananchi, sasa Polisi wajiandae lazima atatokea mwingine kuigiza hii ya kuamua kulipiza kisasi wameandamana wamechoka hakuna linalofanyika

Anonymous said...

mungu awasaidiye sana wamerekani weusi huku hasa hasa wala hoi.yani wanateseka kwenda mbele