Advertisements

Thursday, August 18, 2016

TUME YA MIPANGO YAENDESHA MAFUNZO YA USIMAMIZI YA UWEKEZAJI WA UMMA

Kaimu Naibu katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bi. Lorah Madete Akionesha kitabu cha Mwongozo wa Usimamizi na Utayarishaji wa Miradi ya Uwekezaji katika sekta ya Umma kwa wajumbe wa mafunzo (hawapo pichani), pembeni yake ni Kaimu katibu Mtendani wa Tume ya Mipango Bibi Florence Mwanri.
Wakufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (wenye kompyuta mpakato), wa kwaza kutoka kushoto ni Dkt. Kenneth Mdadila, Katikati ni Dkt. John Mduma, na kulia (mwenye tai) ni Dkt. Jehovaness Aikaeli.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri akifungua mafunzo juu ya Mwongozo wa Usimamizi na Utayarishaji wa Miradi ya Uwekezaji katika sekta ya Umma, pembeni yake ni Kanimu Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bi. Lorah Madete.
Baadhi ya wajumbe Wakifuatilia kinachoendelea wakati wa mafunzo.
Baadhi ya wajumbe Wakifuatilia kinachoendelea wakati wa mafunzo
Mjumbe akitoa machango wake wakati wa mjadala.
Mjumbe akitoa uchambuzi kutoka kwenye kitabu cha Mwongozo wa Usimamizi na Utayarishaji wa Miradi ya Uwekezaji katika sekta ya Umma ambacho ndicho kinachotumika kutolea mafunzo.
Wajumbe Wakifuatilia kinachoendelea wakati wa mafunzo.

Na Adili Mhina
Tume ya Mipango imeanza zoezi la kuwajengea uwezo wataalamu katika kuandaa na kutekeleza miradi ya maendeleo inayotumia fedha za serikali au kwa kushirikiana na Sekta binafsi kwa lengo la kuongeza nidhamu na weledi katika matumizi ya rasilimali za Umma.

Mafunzo hayo yanayoendelea katika moja ya kumbi za ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es salaam na kuendeshwa na wataalamu elekezi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yanalenga kuanda wataalamu ambao watakwenda kutoa mafunzo kwa maofisa wa Serikali walio chini ya idara za Sera na Mipango na zile za uwekezaji katika Wizara, Mikoa, Halmashauri, pamoja na mashirika na taasisi mbalimbali za umma hapa nchini.

Akifungua mafunzo hayo mwanzoni mwa Juma, Kaimu Katibu Mtendani kutoka Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri alieleza kuwa mafunzo hayo yatasaidia kuimarisha utendaji, uwajibikaji na kuleta ufanisi katika matumizi ya rasilimali za umma zinazoelekezwa katika miradi ya maendeleo.

“Shabaha kuu ya mafunzo haya ni kutoa maelekezo ya mchakato na hatua zinazohitajika kufuatwa katika kutayarisha na kutekeleza miradi yote inayotumia fedha za umma au kwa kushirikiana na sekta binafsi,” Alisema Bibi Mwanri.

Kamu Katibu Mtendaji huyo alieleza kuwa kutokana na kukithiri kwa kasoro katika miradi ya maendeleo inayotumia fedha za umma, Serikali kupitia Tume ya Mipango ililazimika kuandaa Mwongozo wa Usimamizi na Utayarishaji wa Miradi ya Uwekezaji katika sekta ya Umma (Public Investment Management Operational Manual) ambao utatumika katika kuandaa, kutekeleza na kusimamia miradi yote inayotumia fedha za umma au kwa kushirikiana na sekta binafsi.

Bibi Mwari alieleza kuwa katika awamu hii ambayo Serikali imejikita katika kujenga uchumi wa viwanda miradi mingi ya maendeleo inatarajiwa kuanzishwa. Hivyo, bila kuwa na uelewa wa pamoja moingoni mwa wadau wanaohusika katika kuandaa, kutekeleza na kusimamia miradi hiyo malengo ya Mpango wa Pili wa Maendeleo hayatafikiwa kama inavyotarajiwa.

“Katika kipindi hiki ambapo bajeti ya maendeleo imeongezeka na kufikia asilimia arobaini ni wazi kuwa miradi mingi ya maendeleo inaanzishwa, hivyo ni lazima kila mtaalamu aelewe kuwa tunawajibu wa kuandaa miradi bora, yenye tija kwa wananchi na inayoendanda na thamani ya fedha zinazotumika,” Alisisitiza Bibi Mwanri.

Bibi Mwanri aliwataka wajumbe wote kuhakikisha wanatumia mafunzo hayo vizuri ili kupata uelewa wa kutosha juu ya mwongozo huo.

Mafunzo hayo ya siku tano yamehudhuriwa na wajumbe kutoka Wizara, Taasisi za Serikali, Wadau wa Maendeleo, Asasi za Kiraia pamoja na Sekta binafsi na yanatarajiwa kuandaa wataalamu bora watakaokwenda katika kanda mbalimbali nchini kutoa mafunzo tarajiwa kwa walengwa.

No comments: