Advertisements

Tuesday, September 20, 2016

KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU ATEMBELEA SHULE ZILIZOATHIRIWA NA MAAFA YA TETEMEKO LA ARDHI KAGERA.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.Prof.Joyce Ndalichako (wa kwanza kushoto) akimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua wakati walipotembelea shule ya sekondari ya Nyakato kujionea athari za maafa ya tetemeko la ardhi Mkoani Kagera Septemba19, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua (wa kwanza kushoto) akizungumza wakati wa ziara yake alipotembelea shule zilizopata athari za maafa ya tetemeko la ardhi mkoani Kagera, wa kwanza kulia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.Prof.Joyce Ndalichako. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua (kulia) akiangalia jengo la ofisi ya walimu lililoathiriwa na maafa ya tetemeko la ardhi katika shule ya sekondari ya Mugeza Mkoani Kagera.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya majengo ya shule ya sekondari ya Ihungo yariyobomoka kutokana na athari za maafa ya tetemeko la ardhi Kagera. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments: