Advertisements

Monday, September 19, 2016

WAZIRI MBARAWA AMTEUA DR MUSA MGWATU KUWA MTENDAJI MKUU WA TEMESA

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame M. Mbarawa(Mb), amemteua Dkt. Musa Mgwatu kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA). 


Dkt. Mgwatu amechukua nafasi ya Mhandisi Marcellin Magesa  ambaye amepangiwa majukumu mengine  Wizarani.

Kabla ya Uteuzi huo Dkt. Mgwatu alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika Hodhi la Rasilimali za Reli (RAHCO). 

Katika hatua nyingine Profesa Mbarawa amemteua Bw. Masanja Kadogosa ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) Kukaimu nafasi ya Mtendaji Mkuu wa RAHCO. 

Uteuzi huo unaanza mara moja.

Imetolewa na 
Eng. Joseph M. Nyamhanga 
Katibu Mkuu (Ujenzi) 
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. 

1 comment:

Anonymous said...

Watanzania mmezidi kupanda titles. Engineer, Dr too much