Advertisements

Tuesday, October 18, 2016

ULEDI MUSSA: KUNA UHURU MKUBWA SANA NDANI YA BUNGE

Na Daudi Manongi,MAELEZO

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Bunge Bw.Uledi Mussa amesema kuwa wabunge wana uhuru mkubwa sana wa kuzungumza ndani ya Bunge.

Katibu Mkuu uyo ameyasema hayo katika kipindi cha TUNATEKELEZA leo jioni kinachoandaliwa na Idara ya Habari MAELEZO na kurushwa na TBC1.

“Bunge letu liko huru sana,liko huru kwa maana wabunge wana uhuru wa kuzungumza na kikatiba yale wanayozungumza ndani ya bunge hawawezi kushitakiwa nje,kwa maana hiyo kuna uhuru mkubwa sana,lakini sasa bunge lenyewe lina Kanuni zake ambapo wewe uliye ndani ya Bunge usimseme mtu ambaye hana fursa ya kuzungumza ndani ya Bunge hivyo bungeni msingi wake mkubwa ni kuzungumza hoja pamoja na kuikosoa,kuishauri serikali na tunafatilia ushauri huu kisekta ili ufanyiwe kazi”Alisema Bw.Uledi

Akizungumzia suala la utoro Bungeni amesema kuwa kwa sasa mahudhurio yanaratibiwa kielektronikali na wabunge watapaswa kuweka dole gumba kwenye mshine ili ajulikane kaingia na kutoka na baadae mahudhurio hayo uchambuliwa na kutumwa katika vyama vyao na hivyo ili litaongeza uwajibikaji binafsi kwa wabunge.


Akizungumzia upande wa hali ya vyama vya siasa nchini katibu mkuu uyo amesema kuwa vyama vingi vya siasa bado ni vichanga na msingi wa vyama vingi hauna muda mrefu hivyo bado vina kazi kubwa ya kujijenga vyenyewe kama taasisi kwenye kuchagua viongozi na Katiba zao.

Aidha katibu Mkuu uyo amevitaka vyama vya siasa kujenga misingi ya kukubali matokeo ya chaguzi zinapofanyika na pia vijenge umoja unaozingatia katiba za vyama vyao.

Bw,Uledi pia amesisitiza kuwa matatizo yanayotokea ndani ya vyama vya siasa yanapaswa kutatuliwa na vyama na wanachama wao wenyewe na kuongeza kuwa migogoro mingi ndani ya vyama ni ya kikatiba na hivyo wasitegemee mtu kutoka nje aje kuwatatulia matatizo yao ingawa ofisi ya waziri mkuu itaendelea kushirikiana na msajili wa vyama vya siasa katika kuwa mlezi wa vyama hivi.

No comments: