Wednesday, December 7, 2016

HEAD, INC ANNUAL GALA DINNER ILIYOFANYIKA HAMPTON INN HOTEL DMV DECEMBER 3, 2016

Baadhi ya Waanzilishi wa HEAD,INC (Health, Education and Development)  wakiwa na Bwana Dismas Assenga(Counselor, Public Affairs), afisa wa ubalozi ambaye alimuwakilisha balozi na ubalozi(Wa tatu kulia) , pamoja na CEO wa African Women Cancer Awareness Association, Bi. Ify Anne Nwabukwu wa pili Kushoto, na Dr. Sylvia Dasi(wa kwanza kushoto) wakiwa tayari kwa shughuli ya Gala Dinner. Lengo na Madhumuni ya HEAD INC ni kusaidia na kushirikiana katika maswala mbali mbali yanayohusiana na huduma za kijamii kwenye nyanja za Afya, Elimu na Maendeleo.

HEAD, INC inawashukuru nyote kwa michango yenu . Pesa zilizopatikana kwenye Gala Dinner zitatumika kwenye kulipia baadhi ya gharama za Tanzania Medical Mission itakayofanyika Summer ya mwakani. Kama unamaswali au mchango wowote wa mawazo, pesa au vifaa wasiliana nasi info@headinc.org au piga 301-613-5165 /301-793-2833/240-813-5563.
Bwana Iddi Sandaly, Mmoja wa Waanzilishi wa HEAD, akimkabidhi Bwana Dismas Assenga zawadi ya Ngao iliyotolewa  na ofisi ya Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa Jumuiya ya Watanzania DMV kwa juhudi zao za kupeleka madaktari Zanzibar mwaka jana 2015.
Bi. Asha Nyanganyi, Mmoja wa Waanzilishi wa HEAD, INC akimkabidhi Bi. Ify Anne Nwabukwu zawadi ya Ngao iliyotolewa  na ofisi ya Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa AWCCA kwa kushirikiana na Jumuiya ya Watanzania DMV kwa juhudi zao za kupeleka madaktari Zanzibar mwaka jana 2015.
















































































No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake