Mvua kubwa ambayo imeambatana na upepo mkali, imesababisha maafa makubwa katika vijiji vitatu vya wilaya ya Butiama mkoani Mara na kusababisha nyumba za kaya zaidi ya mia moja zikiwemo nyumba za ibada kubomolewa vibaya na mvua hiyo iliyoambatana na upepo mkali, huku idadi kubwa ya ekari za mashamba yenye mazao mbalimbali pia yakiathiriwa na mawe yaliambatana na mvua hiyo.
Akizungumza baada ya kukagua athari ambayo imesababishwa na mvua hiyo, mwenyekiti wa kamati ya maafa ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Butiama Bi Annarose Nyamubi, akiwa ameambatana na mwenyekiti wa halmashauri ya Butiama Bw Magina Magesa, wamesema mvua hiyo imesababisha madhara makubwa na kwamba watendaji wa serikali wameanza kufanya tathimini ya kina ili kujua ukubwa wa maafa hayo
Naye diwani wa kata ya Butuguri Bw. Paul Warati, akizungumzia maafa hayo, amesema tathimini ya awali inaonyesha kuwa zaidi ya kaya mia moja,majengo ya taasisi, chakula na mazao mashambani zimeathirika na mvua hiyo iliyoambatana na upepo mkali.
Chanzo: ITV
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake