Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye kijiji cha Mto wa Mbu wilayani Monduli akiwa katika ziara ya mkoa wa Arusha Desemba 4, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa ameshika ngao na Mkuki alivypewa na Mzee wa Mila wa kabila la Wamasai, Laibon Meshuko Ole Mapii (kulia) kabla ya kuwahutubia wananchi kwenye shule ya msingi ya Laibon iliyojengwa na Laibon Ole mapii na kukabidhiwa kwa serikali. Alikuwa katika ziara ya wilaya ya Monduli Desemba 4, 2016. Wengine pichani kutoka kushoto ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa, Jumanne Maghembe, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Arusha, Lekule Laiza.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mzee wa mila wa Kabila la Wamasai, Laibon Meshuku Ole- Mapii kabla ya kuzungumza na wananchi kwenye shule ya Misingi ya Laibon iliyojengwa na Ole- Mapii na kukabidhiwa kwa serikala. Alikuwa katika ziara ya wilaya ya Monduli Desemba 4, 2016.
Baadhi ya wananchi wa Mto wa Mbu wilayani Monduli wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara kijijini hapo akiwa katika ziara wilayani humo Desemba 4, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Maliasili na Utlii, Profes Jumanne Maghembe baada ya kuwahutubia wananchi kwenye shule ya msingi ya Laibon wilayani Monduli Desemba 4, 2016. Katikati ni Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mikutano ya kisiasa ya nje imesharuhusiwa? Au polisi hawakujua kama utakuwepo wakajipanga!?
ReplyDeleteMdau Huu ni wa kiserikali
ReplyDelete