Tanzania inakuwa nchi ya 50 barani Afrika kufikiwa na Shirika la Ndege la
Uturuki baada ya kuongezwa safari tatu kwa wiki kwenda Zanzibar
Shirika la Ndege
la Uturuki limeiongeza Zanzibar katika mtandao wa safari zake kuanzia Desemba
13, 2016. Hivi sasa shirika hilo linafanya safari 49 barani Afrika baada ya
hivi karibuni kuongeza safari ya kwenda Visiwa vya Shelisheli.
Shirika hilo
maarufu barani Ulaya kwa sasa linafanya jumla ya safari 293 duniani kote,
zikiwemo safari 50 kwenye nchi 31 za Afrika.
Likiwa ni
shirika la nne kwa kuwa na mtandao mkubwa wa safari duniani kote kuliko mashirika
mengine, Shirika la Ndege la Uturuki sasa litahudumia miji ya kimataifa 244
ikijumlishwa na Visiwa vya Zanzibar ambavyo ni maarufu kwa biashara ya viungo.
Watumiaji wa ndege za shirika hilo sasa watafurahia uzoefu watakaoupata
kutokana na safari hizo mpya zinazojumuisha miji 20 maarufu duniani kama vile Frankfurt, Muscat,
Munchen, Dubai, Paris, London, Milano, Amsterdam, Zurich, Bombay, Copenhagen,
Stockholm, Rome, Brussels, Berlin, Vienna, Hamburg, Tel-Aviv, Düsseldorf, na Prague.
Safari ya kwanza itazinduliwa
Jumanne, Desemba 13, 2016 na wasafiri wataondoka Istanbul saa 6:30 usiku na
ndege TK567 itakayowasili saa 3:30 asubuhi. Watarudi na ndege hiyo TK567 itakayoondoka
Zanzibar saa 4:25 asubuhi na kuwasili Istanbul saa 11:45 jioni.
Safari za Instanbul – Kilimanjaro – Zanzibar – Istanbul
(IST-JRO-ZNZ-IST) zitakuwa tatu kwa
wiki. Utaratibu wa kuweka mpango wa safari unapatikana kupitia tovuti www.turkishairlines.com
kama ifuatavyo::
Taarifa zaidi kuhusu ratiba ya safari:
Namba ya ndege
|
Kuanzia
|
Siku
|
Kuondoka
|
Kuwasili
|
||
TK 567
|
14 Desemba 2016
|
Jumatatu Jumatano Jumamosi
|
Istanbul
|
20:30
|
3:20 (+1)
|
Kilimanjaro
|
TK567
|
15 Desemba 2016
|
Jumanne Alhamis Jumapili
|
Kilimanjaro
|
04:15
|
5:30
|
Zanzibar
|
TK 567
|
15 Desemba 2016
|
Jumanne, Alhamis Jumapili
|
Zanzibar
|
06:25
|
13:45
|
Istanbul
|
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake