Wauza mitumba katika Soko la Tandika wakiwa wamepozi kwa furaha baada ya Rais Dk.John Magufuli kuwaruhusu kufanya biashara zao pasipo kubugudhiwa.
Na Dotto Mwaibale
WAFANYABIASHARA ndogo ndogo wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam wamempongeza Rais Dk.John Magufuli kwa kuwaruhusu kuendelea kufanyabiashara zao bila ya kubugudhiwa na kumtaja kuwa ni kiongozi wa wanyonge na watu wa chini.
Kauli hiyo wameitoa leo asubuhi wakati wakitoa maoni yao baada ya Rais kutoa tamko hilo Dar es Salaam jana.
Mchuuzi wa urembo katika Soko la Tandika Kamtanda Hamisi alimshukuru rais kwa kuwaruhusu na kuwajali watu wa chini.
"Nawaomba wafanyabiashara wenzangu ruhusa ya rais isiwe kibali cha sisi kuanza kupanga biashara zetu barabarani tufuate sheria" alisema Hamisi.
Muuza mitumba Hassan Bakar alisema Rais Magufuli yupo vizuri tunakila sababu ya kumpongeza katika jambo hilo la kuwatetea wanyonge yupo katika mstari ulionyooka na tumeteseka kwa miaka mingi.
Juma Abdul alisema anafuraha kwa uamuzi huo wa rais kwani ametimiza ahadi yake aliyoitoa wakati wa uchaguzi mkuu.
"Tulitukanwa sana na kunyang'anywa bidhaa zetu sasa baba yetu Magufuli ametuona na kutuondoa kwenye mateso hayo" alisema Abdul.
Mfanyabiashara wa viatu Evord Lyimo alisema walikuwa wakiishi kama digidigi na kupoteza bidhaa zao baada ya kuchukuliwa na mgambo sasa vitendo hivyo vimekoma kupitia kwa rais wetu tunampongeza kwa hatua hiyo.
Salum Mwinyimkuu alisema Rais yupo sahihi kwa hatua hiyo, kazi hii tunayoifanya ndio ajira yetu inayotuwezesha kuishi na familia zetu.
Mfanyabiashara wa matunda Salum Ramadhan alisema wanamshukuru rais kwa ruhusa hiyo hivyo akatoa mwito kwa wenzake kuzingatia sheria ya kutofanya biashara barabarani na kuzuia vyombo vya moto visipite.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake