Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Godwin Gondwe na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe, wakisalimia wananchi wa Kata ya Segera
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni BW. William Makufwe akizungumza na wananchi wa Kata ya Segera kwenye maadhimisho hayo.
Wananchi Wilayani Handeni
wametakiwa kufuata maadili katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ili kujihahakikishia
huduma bora za jamii.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu
wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe alipokuwa akisikiliza kero za wananchi
wa Kata ya Segera iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Handeni jana katika
maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki
za Binanadamu Kiwilaya yaliyoandaliwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na
Rushwa nchini (TAKUKURU).
Gondwe alisema “
Maadli ni imani njema, sehemu yoyote yenye maadili haki za binadamu hufuatwa,
hakuna ardhi itakayouzwa kiholela, wagonjwa watatibiwa vizuri kwenye vituo vya
afya, wageni wataingia kwenye maeneo yetu kwa kufuata taratibu za nchi na
shughuli zote zitafanyika kwa misingi ya Haki”.
Aidha aliwataka watumishi wa
umma na wananci kwa ujumla kufuata sheria, taratibu na kanuni pasipo kujali
wala kubagua rangi au cheo cha mtu yeyote. Alisema kuwa Rushwa ni adui wa
haki na kuwataka kuikataa kwa kauli na
vitendo.
Wakati huohuo Mkuu wa Wilaya
ya Handeni alivunja baraza la Ardhi la Kata kwa kulalamikiwa na wananchi
kutotekeleza maajukumu yeke na kuwaagiza TAKUKURU Wilaya ya Handeni kulichunguza
hadi ifikapo mwishoni mwa mwezi Januari 2017, na mapungufu yoyote
yatakayobainika basi hatua za kisheria
zichukue mkondo wake maramoja.
Vilevile aliwaaagiza Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji
kusimamisha shughuli zote za kilimo zinazofanywa kwenye msitu wa hifadhi ya
kijiji
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe aliwataka Maafisa Watendaji
na wenyeviti wa Vijiji kusimamia miradi yote ya maendeleo kwa maadili na uadilifu kutokana na dhamana kubwa
waliyonayo kwenye maeneo yao ya kiutawala. Vilevile aliwataka kusoma tarifa za mapato na matumizi na kuwa
tayari kujibu hoja za wananchi kuhusu taarifa za mapato na matumizi. “Mtendaji
atakayeshindwa kusoma taarifa za mapato na matumizi atakua amejiondoa mwenyewe
kwenye nafasi yake” Alisema Makufwe.
Mkuu wa TAKUKURU Wilaya Bi.
Esta Mulima, alisema TAKUKURU itaendelea kupambana na Rushwa kikamilifu na
kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu madhara ya Rushwa. Aliwataka wananchi
kufichua vitendo vya rushwa vinapotokea au dalili za vitendo hivyo ili hatua
ziweze kuchukuliwa.
Maadhimisho ya siku ya
Maadili na Haki za Binadamu hufanyika kila tarehe 10 Disemba Kitaifa, na
Wilayani hapa yalifanyika tarehe 8 Disemba
kutokana na Muingiliano wa Majukumu yakiongozwa na kauli mbiu isemayo.
“kujenga na kukuza maadili, haki
za binadamu, uwajibikaji, utawala bora na Mapambano dhidi ya Rushwa”.
Alda Sadango
Afisa habari
Halmashauri ya Wilaya ya
Handeni
9 Desemba 2016.
Mkuu wa TAKUKURU Wilaya Bi. Esta Mulima akizungumza na wananchi wa Kata ya Segera kwenye maadhimisho.
Baadhi ya Maafisa wa TAKUKURU, Wilaya wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya.
Baadhi ya wananchi wa kata ya Segera .
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake