Monday, December 5, 2016

WANAWAKE WAJASIRIAMALI MASOKONI WAMETAKIWA KUWA NA MSHIKAMANO

 Mwakilishi Mkazi wa Taasisi ya Sura Mpya na Sauti Mpya Tanzania (NFNV), Emma Kawawa (kulia), akizungumza na wanawake wafanyabiashara katika masoko ya Ilala na Temeke wakati akifunga mkutano wa kupanga na kuweka mikakati ya vikundi vya umoja na umoja wa kitaifa wa wanawake (Uwawasota) kwa mwaka 2017 uliofanyika Hoteli ya  Dreamer Buguruni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake katika Soko la Mchikichini, Betty Mtewele (kulia), akizungumza katika ufungaji wa mkutano huo.
Ofisa Mradi na Mwanasheria wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Mussa Mlawa (kushoto), akiteta jambo na Ofisa Uwezeshaji Jamii Kiuchumi wa Shirika hilo, Theresia Jeremia .
Wanawake wajasiriamali wakiwa kwenye mkutano huo.
Ofisa Mradi na Mwanasheria wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Mussa Mlawa (kulia), Mwezeshaji sheria masokoni, Consolatha Cleophas na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake katika Soko la Mchikichini, Betty Mtewele wakifuatia kwa karibu mafunzo hayo.
Mwezeshaji wa sheria katika Soko la Temeke Sterio, Batuli Mkumbukwa akiandika changamoto na  za uendeshaji na usimamizi wa umoja kwenye masoko.
Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.
Makofi yakipigwa baada ya hutuba ya mgeni rasmi Emma Kawawa.
Usikivu katika mkutano huo.
Mafunzo yakiendelea,
Mgeni rasmi Emma Kawawa akifunga mafunzo hayo.

Tabasamu wakati wa mafunzo hayo.
Picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Picha  hiyo 
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na viongozi.


Na Dotto Mwaibale

WANAWAKE Wajasiriamali nchini wametakiwa kuwa na mshikamano, uthubutu, na upendo ili kusonga mbele katika shughuli zao za kiuchumi.

Mwito huo ulitolewa na Mwakilishi Mkazi wa Taasisi ya Sura Mpya na Sauti Mpya Tanzania (NFNV), Emma Kawawa ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati akifunga mkutano wa kupanga na kuweka mikakati ya vikundi vya umoja na umoja wa kitaifa wa wanawake (Uwawasota) kwa mwaka 2017 uliofanyika Hoteli ya Dreamer Buguruni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

"Mkitaka kusonga mbele kiuchumi kupitia ujasiriamali wenu kama wanavyo fanya wanawake wenzetu katika nchi mbalimbali duniani mnapaswa kuwa na uthubutu, kupendana, kuacha majungu, kutunza muda  na kushirikiana" alisema Kawawa.

Ofisa Mradi na Mwanasheria wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Mussa Mlawa alisema lengo la mkutano huo ni kuwakutanisha viongozi wa vikundi vya umoja wa wanawake kwenye masoko ya Manispaa  ya Ilala na Temeke ili kuweza kujadili changamoto za uendeshaji na uimarishaji wa umoja masokoni kwa mwaka 2017.

"Malengo mengine ya mkutano huu ni kutengeneza mpango kazi wa kufufua na kuimarisha umoja masokoni kwa mwaka 2017, kupeana mrejesho wa usajili wa umoja wa kitaifa (Uwawasota) na kupokea taarifa ya kamati ya uhamasishaji wa umoja kwa mwaka 2016" alisema Mlawa.

Ofisa Uwezeshaji Jamii Kiuchumi wa Shirika hilo, Theresia Jeremia alisema mkutano huo uliwahusisha wanawake wajasiriamali kutoka masoko sita ya katika manispaa za Temeke na Ilala ambayo ni Gezaulole, Tabata Muslimu, Ferry, Temeke Sterio na Mchikichini.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake