Saturday, December 3, 2016

WWaziri Mahiga ashiriki maadhimisho ya siku ya Kitaifa ya Umoja wa Falme za Kiarabu


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu nchini Mhe.Abdulla Ibrahim Ghanim Alsuwaidi alipowasili katika ofisi za ubalozi huo kushiriki sherehe ya madhimisho ya miaka 45 ya muungano.Tanzania na UAE zimepiga hatua kubwa za ushirikiano hususan ya kiuchumi ambapo kwa takwimu za Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) hadi Juni, 2015 makampuni 67 ya uwekezaji kutoka UAE yamewekeza hapa nchini katika sekta mbalimbali wenye thamani ya USD 497.12 Millioni na kuajiri Watanzania 9,044. Taifa la Umoja wa Falme za Kiarabu unaundwa na falme saba ambazo ni Abu Dhabi, Dubai, Sharjah, Ras Al Khaimah, Fujairah, Ajman na Umm al-Quwain

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Taifa la Umoja wa Falme za Kiarabu Mhe.Abdulla Ibrahim Ghanim Alsuwaidi wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka 45 ya muungano wa falme hizo

Mhe.Waziri Balozi Dkt.Mahiga akivalishwa skafu maalum

Mhe.Waziri Balozi Dkt. Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mhe.Abdulla Ibrahim Ghanim Alsuwaidi

Wageni waalikwa wakifuatilia jambo

Balozi wa Taifa la Umoja wa Falme za Kiarabu Mhe.Abdulla Ibrahim Ghanim Alsuwaidi akizungumza wakati wa maadhimisho

Mhe. Waziri Balozi Dkt. Mahiga akitoa hutuba fupi wakati wa maadhimisho ya sherehe hizo

Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Abdalla Kilima akisalimiana na Mhe. Balozi wakati wa sherehe za maadhimisho
Tanzania na Umoja wa Nchi za Kiarabu (UAE) zimepiga hatua kubwa za ushirikiano hususan wa kiuchumi ambapo kwa takwimu za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) hadi Juni, 2015 Makampuni 67 kutoka UAE yamewekeza hapa nchini katika sekta mbalimbali kwa mtaji wa thamani ya Dola za Marekani milioni 497.12 na kuajiri Watanzania zaidi ya 9,044. 

Hayo yalibainishwa jana katika sherehe za kuadhimisha Siku ya Kitaifa ya UAE zilizofanyika jijini Dar Es Salaam ambapo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga alikuwa Mgeni Rasmi. 

Tanzania na UAE zinatarajiwa kufanya Mkutano wa Kwanza wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPC) ambao utakuwa chachu ya kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizi mbili hususan ya kiuchumi. 

Akiongea katika hafla hiyo, Mhe. Waziri alilipongeza taifa hilo kwa kuadhimisha siku yake ya Kitaifa ikiwa imepiga hatua kubwa ya kimaendeleo ya kichumi, kijamii na kisiasa. Mhe. Waziri alisema kuwa siku hiyo ni inatoa fursa pia ya kutathmini mahusiano mazuri yaliyopo baina ya Tanzania na UAE. 

Kwa upande wake, Balozi wa UAE hapa nchini, Mhe. Abdulla Ibrahim Ghanim Alsuwaidi aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mkubwa inayotoa kwa Ubalozi huo ambao unamwezesha kutekeleza majukumu yake kwa wepesi ikiwa ni pamoja na kuimarisha mahusiano ya nchi hizi mbili. Mhe. Balozi aliahidi kuendeleza ushirikiano huo hususan katika kutimiza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda. 

Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) unajumusha falme saba ambazo ni Abu Dhabi, Dubai, Sharjah, Ras Al Khaimah, Fujairah, Ajman na Umm al-Quwain huadhimisha siku yake ya Kitaifa tarehe 02 Disemba ya kila mwaka tokea mwaka 1971.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake