Tuesday, January 17, 2017

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LATOA ELIMU YA KINGA NA TAHADHARI YA MAJANGA YA MOTO.

Sajini Simon Sadala wa kituo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mbeya (Mbele) akitoa elimu ya Kinga na Tahadhari dhidi ya majanga ya moto katika taasisi ya kifedha(Access Bank) tawi la Mbeya.
Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa mbeya wakiwa kwenye picha ya pamoja na Watumishi wa benki ya Access tawi la mbeya mara baada ya kumaliza kupata mafunzo hayo mapema leo asubuhi (Picha na Jeshi la Zimamoto)

Katika kuendeleza juhudi za kupunguza na kutokomeza majanga ya moto yanayoikabili jamii, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limeendelea na zoezi la utoaji elimu juu ya Kinga na Tahadhari dhidi ya Majanga ya Moto Nchini.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linajukumu kubwa la kutoa huduma kwa jamii katika Nyanja mbalimbali zikiwemo Kuokoa maisha ya watu na mali zao, Kuzima moto, Kutoa elimu ya kinga na tahadhari ya majanga moto, Kufanya ukaguzi wa tahadhari na kinga ya moto, Kusoma ramani za majengo na kutoa ushauri, Kutoa huduma ya kwanza katika majanga na ajali barabarani, Kutoa mafunzo ya kukabiliana na majanga ya moto, Kufanya uchunguzi kwenye majanga ya moto na Kutoa huduma za kibinadamu.

Huduma ya Zimamoto inatolewa bure na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji hivyo basi tunawaasa wananchi kutumia namba ya dharura 114 mara tu wapatwapo na majanga ili kurahisisha uokoaji wa Maisha na Mali kwa haraka.Kwa kuzingatia majukumu hayo Askari wa kituo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mbeya wamewapatia elimu ya kukabiliana na majanga ya moto Watumishi wa banki ya Access tawi la Mkoa wa mbeya.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake