ANGALIA LIVE NEWS

Monday, January 16, 2017

JPM awateua Kabudi, Bulembo kuwa wabunge

Alhaji Abdallah Bulembo akisalimiana na Rais John Magufuli.Picha ya Maktaba

By Mwandishi Wetu, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co

Dar es Salaam. Rais John Pombe Magufuli, leo amewateua Profesa Palamagamba Kabudi na Alhaji Abdallah Bulembo kuwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Taarifa iliyoletwa na Kitengo cha Mawasiliano cha Ikulu leo, imeeleza kuwa wabunge hao wateule wataapishwa kwa taratibu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia, Rais Magufuli amemteua Benedicto Martin Mashiba kuwa Balozi.

Kituo cha kazi na tarehe ya kuapishwa kwa Balozi Mteule Benedicto Martin Mashiba vitatangazwa baadaye.

1 comment:

Anonymous said...

Hongera zao wateuliwa na ninamatumaini lilenfungunla mgawo wa millioni kumi wametengewa na watapewa bahasha siku ya kuapishwa. Salaam.