Sunday, January 15, 2017

MWANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO GAZETI LA UHURU AMINA ATHUMAN AFARIKI DUNIA

Mwandishi wa habari za Michezo wa Gazeti la Uhuru, Amina Athuman (pichani) amefariki Dunia leo asubuhi katika Hosptali ya Mnazi Mmoja mjini Zanziba alikokuwa amelazwa.

Amina alilazwa Hospitalini hapo baada ya kuzidiwa (kushikwa na uchungu) kutokana na ujauzito na kukimbizwa kupata huduma katika hospitali hiyo ambpo alijifungua mtoto wa Kiume (Bahati mbaya) na yeye akaendelea kupatiwa matibabu hadi ulipomkuta umauti asubuhi ya leo.

Amina alikua mjini Zanziba kikazi alipokwenda kuripoti mashindano ya Kombe la Mapinduzi, ambapo alikuwa arejee jijini Dar es Salaam jana.

Mungu ilaze roho ya Marehemu Amina Athuman mahala pema peponi, Amina

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake