Monday, January 16, 2017

Polisi Geita Wamkamatwa Edward Lowassa

GEITA: Waziri Mkuu wa zamani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa na viongozi wengine wa chama hicho amekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Geita leo Januari 16, 2017.
Chanzo cha taarifa hiyo kimeeleza kuwa, Lowassa na wenzake alipita kituo cha mabasi cha zamani cha Geita wakitokea mkoani Kagera kwenye ziara kuelekea kwenye kampeni za uchaguzi Kata ya Nkome, ambapo walisimamishwa na wananchi waliokuwepo eneo hilo, baada ya kushuka kwenye gari kwa ajili ya kusalimiana nao, polisi waliwakamata na kuwampeleka Kituo Kikuu cha Polisi Geita.

Mpaka sasa haijaelezwa kosa lililosababisha kukamatwa kwake.
Alipopigiwa simu na Mtandao wa Global Publishers, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Geita, ACP Mponjoli Lotson alisema alikuwa nje ya mji wa Geita, hivyo apewe muda ili afuatilie na kujua sababu.
GPL

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake