Mbunge wa viti maalumu
mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rita Kabati akimpigia kampeni mgombea udiwani wa kata ya Igombavanu na kuwataka wapinzani
kusahua kama watashinda katika kampeni za kuwania kiti cha udiwani katika kata
ya Igombavanu tarafa ya Sadani wilayani Mufindi mkoani iringa zinaendelea
kupamba moto huku uchaguzi ukitarajiwa kufanyika siku ya tarehe 22 /01 /2017.
katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi Jimson Mhagama amewataka
wananchi kuwataa kabisa wapinzani kwa kuwa si waadilifu katika kuleta maendeleo
Mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazini Mahamood Mgimwa aliwaomba wapiga
kura kumpigia kura nyingi diwani wa chama cha mapinduzi Rashidi Mkuvasa ili awe
diwani wa kata ya Igombavanu na kuwa kiungo muhimu kuwaletea wananchi maendeleo
Mgombea udiwani wa kata hiyo kupitia chama cha mapindizi (CCM) Rashidi
Mkuvasa amesema wananchi wanapaswa kuwa makini na mbinu chafu zinazotumiwa na
wapinzani wake kwa kuwalaghai wananchi kwa kununua vitambulisho
Na fredy mgunda,Iringa
MBUNGE wa viti maalumu
mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rita Kabati amewataka wapinzani
kusahua kama watashinda katika kampeni za kuwania kiti cha udiwani katika kata
ya Igombavanu tarafa ya Sadani wilayani Mufindi mkoani iringa zinaendelea
kupamba moto huku uchaguzi ukitarajiwa kufanyika siku ya tarehe 22 /01 /2017.
Akizungumza wakati wa
mkutano wa kampeni uliofanyika katika kijiji cha Makongomi mbunge Kabati
aliwaambia wananchi kuwa jimbo la Mufindi kaskazini na wilaya ya Mufindi kwa
ujumla ni ngome ya chama cha mapinduzi (CCM) hivyo wapinzani wasipoteze muda wa
kupiga kampeni kwa kuwa hawawezi kushinda chaguzi zote za jimbo hilo.
Kabati alisema kuwa wananchi
wa wilaya ya Mufundi bado wanakipenda chama cha mapinduzi na wanahakika
watashinda kutokana na mapokeo mazuri kutoka wapiga kura ambao wanazikubali
sera za chama cha mapinduzi na wanaendelea kumuamini rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
“Mimi nikiangalia naona
nyuso za furaha tu hapa na nimepemda kuwa mmetukikishia kushinda uchaguzi huu
basi furaha yangu itakuwa siku ile diwani wetu kutoka chama cha mapinduzi
anatangazwa kuwa mshindi kwa kura nyingi,nawapenda na naomba mkipe kura nyingi
chama cha mapinduzi”.alisema Kabati
Naye mbunge wa jimbo la
Mufindi kaskazini Mahamood Mgimwa aliwaomba wapiga kura kumpigia kura nyingi
diwani wa chama cha mapinduzi Rashidi Mkuvasa ili awe diwani wa kata ya
Igombavanu na kuwa kiungo muhimu kuwaletea wananchi maendeleo.
“Jamani nipeni huyu diwani
ili tuendelee kufanya maendeleo kwa kuwa mimi mnaniamini basi naomba mpeni kura
nyingi na kuondokana na maneno machafu kutoka kwa wapinzani kwani wapinzani
hawana jipya saizi”.alisema Mgimwa
Kwa upande wake katibu wa
chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi Jimson Mhagama amewataka wananchi kuwataa
kabisa wapinzani kwa kuwa si waadilifu katika kuleta maendeleo,alimalizia kwa
kuwaomba wananchi wa kata hiyo kumchagua Rashidi Mkuvasa kwa kuwa ni kiongozi
mzuri na atawaletea maendeleo wananchi wa kata hiyo.
“Tumeona wagombea wengi
wakija hapa kupiga kampeni na kuomba kura kwa njia ya matusi na kuhamasisha
kutomchagua kiongozi furani pasipo kutaja au kuongelea hata hoja za msingi
kwanini wanaomba kura zetu” alisema Mhagama
Mgombea udiwani wa kata hiyo
kupitia chama cha mapindizi (CCM) Rashidi Mkuvasa amesema wananchi wanapaswa
kuwa makini na mbinu chafu zinazotumiwa na wapinzani wake kwa kuwalaghai
wananchi kwa kununua vitambulisho au kunakili namba za vitambulisho hivyo
.
“Tuwakatae viongozi wa namna
hiyo kwa kuwa lengo lao ni kutaka kununua uongozi kwa nguvu ya pesa na kuwa wao
sio chaguo la wanachi hivyo wananchi msithubutu kufanya hivyo mtapoteza haki
yenu ya msingi na hamtampata kiongozi atakaye waletea maendeleo”.alisema
Mkuvasa
Aidha wananchi wa kata ya
Igombavanu katika jimbo la Mufindi Kaskazini wamempongeza mgombea udiwani wa
kata kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) Rashidi Mkuvasa kwa kufanya
kampeni za kistaarabu na kuwapa matumaini kuwa atakuwa kiongozi mzuri na
kuwaletea maendeleo katika kata hiyo.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake