Tuesday, January 17, 2017

SERIKALI YAAHIDI KUFUNGUA DUKA LA DAWA KWA KILA MKOA

Na Mussa Mbeho ,katavi

Serikali imeweka mkakati wa kufungua duka la dawa muhimu kwa kupitia MSD kwenye kila hospitali ya kila mkoa hapa Nchini ili kuondoa tatizo la vifaa tiba na dawa na kuwapunguzia wanachi gharama ya ununuzi wa dawa.

Kauli hii ilitolewa hapo jana na Waziri Kassim Majaliwa wakati alipokuwa akifungua duka la dawa la MSD katika Hospitali ya Manispa ya Mpanda Mkoani Katavi .

Alisema Serikali imeweka mkakati wa mpango wa kufungua duka la dawa kwenye kila Mkoa hapa Nchini ili kukailiana na tatizo la upungufu wa vifaa tiba na dawa linazozikabili hospitali mbalimbali hapa Nchini .

Majaliwa alieleza kuwa MSD itakapo kuwa imekamilisha ufunguzi wa maduka ya madawa kwenye kila mkoa wakakuwa watakuwa wamewapunguzia wananchi gharama ya kubwa .

Alifafanua kuwa Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa Mikoa saba ambayo MSD wamefungua duka la dawa na mpango huo utaendelea kwenye Hospitali nyingine za Mikoa hapa Nchini .

Alieleza kwa sasa Serikali inazo pesa nyingi za kutosha ambazo wamezikamata kutoka kwa mafisadi ambazo wamepanga kuzipeleka katika elimu afya na maeneo mengine wanayoyapa kipaumbele .

Hivyo aliwaomba Watanzania kuwaunga mkono kwenye swala zima la kupambana na ufisadi hapa nchini kwani mapambano hayo ni ya Wanzania wote.

Waziri Mkuu Majaliwa alizitaka Wizara za afya na Tamisemi kukaa pamoja na kuona na kupanga namna ya kuendesha maduka ya hayo yatakayokuwa yamefunguliwa na MSD kwenye Hospitali za Mikoa .

Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laulent Bwanakunu alisema lengo la kufungua maduka hayo ni kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi , ili kuhakikisha kuwa wanapata dawa zenye ubora na kwa bei nafuu.

Maduka hayo yanahumuhimu wake hasa maeneo ya Wilayani na endapo MSD itapewa fedha inaweza kufungua maduka kwenye Hospitali zote za rufaa za mikoa lakini wanapenda hospitali hizo ziendeshe zenyewe .

Alisema maduka hayo yataongeza mapato ya hospitali kama ambavyo maelelezo yaliyotolewa na serikali kuwa Halmashauri zifungue maduka hayo na MSD itakuwa tayari kuwapatia mali yani dawa na vifaa tiba .

Mkurugenzi huyo wa MSD alisema kuanzishwa kwa duka hilo Mkoani Katavi kutaongeza upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa wagonjwa hasa dawa ambazo ambazo hazimo katika orodha zilizoidhinishwa na Serikali kutumika katika vituo vyake vya kutolea huduma za afya NEMLIST lakini zimehizinishwa kutumika na mamlaka husika likiwemo shirika la afya Duniani .

Alisema dawa na vifaa tiba vilivyomo katika orodha ya mfuko wa Bima ya afya pia zitapatikana katika duka hilo kwa bei nafuu hivyo kuondoa usumbufu wa wagonjwa wa kwenda kuzitafuta katika maduka ya mbali na kwa bei ghali .

Alieleza duka hilo la dawa lililofunguliwa Mkoani Katavi litasaidia pia kwa Mikoa ya Rukwa na Kigoma ambao watakuwa wananunua dawa kwenye duka hilo kwa ajiri ya hospitali zao na vituo vya afya .

MWISHO

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake