Makamu Mwenyekiti Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Bw. William Kalaghe Akimueleza jambo Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye alipofanya ziara na kuongea na watumishi wa Shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Taifa (TBC) Dkt. Ayoub Rhioba akimueleza jambo Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye wakati alipokutana na uongozi wa Shirika hilo wakati wa ziara na kuongea na watumishi wa Shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye akiongea na uongozi wa Shirika la Utangazaji Taifa (TBC) alipofanya ziara ya kuongea na watumishi wa Shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye akitembelea maeneo mbalimbali ya studio za Shirika la Utangazaji Taifa (TBC) wakati wa ziara katika shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye akisaini kitabu cha wageni wakati wa Ziara katika shirika wa Shirika la Utangazaji Taifa (TBC) leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Taifa (TBC) Dkt. Ayoub Rhioba akitoa taarifa ya utekelezaji wa shirika hilo kwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye ambapo alimueleza mipango ya shirika hilo katika kuhakikisha linakuwa mfano barani Afrika.
Makamu Mwenyekiti Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Bw. William Kalaghe akimkaribisha Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye kuongea na wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Taifa (TBC) alipofanya ziara katika shirika hilo.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye akiongea na wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Taifa (TBC).
Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Taifa (TBC) wakimueleza Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye changamoto za kiutendaji zinazolikabili shirika hilo wakati wa ziara katika shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Taifa (TBC) wakimsikiliza Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa TBC na wafanyakazi wa Shirika hilo.
(PICHA NA IDARA YA HABARI/WHUSM)
Na Shamimu Nyaki-WHUSM
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye amewataka wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kufanya kazi kwa ari ili kuhakikisha linakuwa mfano Barani Afrika katika kuhabarisha umma.
Waziri Nape ameyasema hayo leo alipofanya ziara katika Shirika hilo ili kuona utendaji kazi pamoja na kuona changamoto mbalimbali zinazolikabili Shirika hilo.
“Fanyeni kazi kwa bidii na uadilifu kwa kutoa taarifa za ukweli na zenye uhakika kwa watazamaji puuzeni propaganda zinazoenezwa mtaani kuwa Shirika hili limepoteza Watazamaji na wasikilizaji kwa manufaa ya Taifa letu”.Alisema Waziri Nape.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Dkt.Ayoub Ryoba ameeleza kuwa Shirika linaendelea kuongeza wasikilizaji na watazamaji ambapo kuanzia mwaka 2012 hadi 2016 limeongeza mitambo kutoka kumi na mbili hadi hadi kumi na tisa iliyofungwa Mtwara,Rombo,Mbambabei na Tarime.
Aidha, Dkt Ryoba ameongeza kuwa Shirika hilo bado linaendelea kuwa katika historia ya Kuwa Shirika lililohabarisha umma juu ya Jitihada za Serikali ya Tanzania katika Ukombozi wa Bara la Afrika pamoja na kuendelea kukuza lugha ya Kiswahili kupitia kipindi cha malenga wapya.
“Shirika letu linaendelea kutoa habari, elimu na burudani zinazozingatia muktadha wa Utamaduni wa Nchi yetu ambapo kwa kipindi cha mwaka jana tumekuwa tukirusha matukio mubashara kupitia mitandao ambayo yana wafuatiliaji zaidi ya million tano.” Alisema Dkt.Ryoba.
Shirika hilo linaendelea kuwafikia watazamaji na wasikilizaji wengi zaidi ndani na nje ya nchi kwa kuendelea kuweka mikakati ya kuongeza vituo vingi zaidi.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake