ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, January 18, 2017

WAZIRI PROFESA MBARAWA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA SHIRIKA LA POSTA


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Profesa Makame Mbarawa akiwasili Ofisi za Posta Kuu ya Shirika la Posta maeneo ya Posta Mpya wakati alipofanya ziara ya kushtukiza Dar es Salaam leo. Kulia ni Postamasta Mkuu, Fortunatus Kapinga.(Picha zote na Kassim Mbarouk www.bayana.blogspot.com )
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akipatiwa maelezo na Meneja wa Posta Mkoa wa Dar es Salaam, Margret Mlyomi (katikati), wakati alipofika katika ziara ya kushtukiza kwenye Ofisi za Shirika la Posta, Posta Kuu jijini Dar es Salaam leo kuangalia shughili mbalimbali zinavyofanyika ofisini hapo.
Mkuu wa Kitengo cha Usalama cha Shirika la Posta Tanzania, George Mwamgabe (kushoto), akimpatia maelezo Waziri Profesa Mbarwa kuhusu mambo ya usalama kwenye mtandao wa shirika hilo. Kulia ni Kaimu Meneja Mkuu wa Shirika la Posta, shughuli za biashara, Janeth Msofe.
Waziri Profesa Mbarwa, akimsikiliza mteja wa shirika hilo, Mhandisi Nungu Allanus kutoka DIT, kuhusu ubora wa utoaji huduma wa shirika. 
Waziri Profesa Mbarwa (kulia), akisikiliza maelezo kutoka kwa Msaidizi Meneja wa Fedha na Huduma wa shirika hilo, wakati alipotembelea kitengo kipya cha kutolea huduma mbambali za kifedha cha Jamii Centre. Katika Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika, Dk. Harun Kondo. 
Waziri Profesa Mbarwa (kushoto), akimweleza jambo Meneja wa Posta Mkoa wa Dar es Salaam, Margret Mlyomi (katikati), wakati akitembelea Posta Kuu, maeneo ya Posta Mpya jijini Dar es Salaam leo, wakati wa ziara hiyo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Usalama cha Shirika la Posta Tanzania, George Mwamgabe.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta, Dk. Harun Kondo (katikati), akimweleza jambo Waziri Profesa Mbarawa, akitembelea vitengo mbalimbali vya Ofisi za Posta Kuu jijijini katika ziara hiyo.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, akizungumza wakati Waziri Profesa Mbarawa alipokutana na wafanyakazi na kuzungumza nao Makao Makuu ya shirika hilo, wakati akimaliza ziara yake hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta, Dk. Harun Kondo (kulia), akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri Profesa Mbarawa, kuzungumza na wafanyakazi, Makao Makuu ya shirika hilo, wakati wa kumaliza ziara yake hiyo.
Waziri Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Posta, Makao Makuu ya shirika hilo, wakati wa ziara yake hiyo.
Ofisa Mwandamizi wa Shirika la Posta, Makao Makuu, David Hango, akizungumza wakati akimweleza Waziri Profesa Mbarawa baadhi ya changamoto zinazolikabili na kukwamisha shirika hilo katika kupiga hatua za kimaendeleo.
Mmoja wa wafanyakazi wa shirika hilo kutoka Chama cha Wafanyakazi cha Tewuta, Ahmed Kaumo, akimweleza Waziri Profesa Mbarawa baadhi ya changamoto ambazo angependa kuwa na kikao cha pamoja cha Viongozi wa shirika hilo na wa chama hicho cha wafanyakazi katika kukabiliana nazo ili kulikwamua shirika hilo.
Mmoja wa wafanyakazi wa shirika hilo, upande wa Masoko, Joyce Kagose, akimweleza Waziri Profesa Mbarawa changamoto mbalimbali zinazolikabili shirika hilo.
Mmoja wa wafanyakazi wa zamani wa shirika hilo, akimweleza kwa uchungu Waziri Profesa Mbarawa jinsi changamoto wanazozipata kutoka kwa baadhi ya watendaji wa shirika hilo, ambao hujifanya wasomi na kuwazarau wale wa zamani kutokana na elimu zao.
Waziri Profesa Makame Mbarawa (katikati), akisikiliza maelezo yaliyokuwa yakitolewa na wafanyakazi hao.
Waziri Profesa Makame Mbarawa, akijibu baadhi ya hoja na ushauri wa wafanyakazi wa shirika hilo, wakati wa ziara yake hiyo.

2 comments:

Anonymous said...

Wizi wa packages/parcel za watu umekithiri posta.

Anonymous said...

Msafiri anapo acha mzigo airport kwa sababu zozote zile za kushidwa kulipia na kupewa siku 7 za kulipia wakati amesha ondoka,na kudai kama una jeuri nenda mahakamani, maneno hayo yanaleta uchungu sana,unafika unakoenda ukipiga simu unaambiwa vitu vilipigwa mnada inauma sana sana, sikushidwa kulipia gharama za kuhifadhi.