Mbunge wa
viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) akikinga maji kwenye ndoo kuashiria sasa kisima cha maji kimefunguliwa na kuanza kutumia kwa wakazi wa mtaa wa Igungandembwe manispaa ya Iringa akiwa na diwani wa kata ya Nduli Bashir Mtove wakati wa uzinduzi wa kisima hicho.
Mbunge wa
viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati(CCM) akiangalia maji waliyokuwa wanatumia wananchi mtaa wa Igungandembwe manispaa ya Iringa.
Na haya ndio maji waliyokuwa wanatumia wananchi wa mtaa wa Igungandembwe
manispaa ya Iringa kabla ya kujimbiwa kisima
Na Fredy Mgunda, Iringa.
Wananchi wa mtaa wa Igungandembwe
manispaa ya Iringa wamemshukuru mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta
Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) na diwani wa kata ya Nduli Bashir
Mtove kwa msaada wa kuwachimbia kisima cha maji safi na salama.
Wakizungumza na blog hii
wananchi hao wamesema kuwa wanatakribani miaka hamsini na tatu (53) hawajawahi
pata maji masafi na salama.
“Angalia maji haya machafu
ndio tulikuwa tunakunywa na kupikia ila mungu alikuwa anatusaidia tu kutuepusha
na magonjwa mbalimbali kiukweli leo tunafuraha sana kuanza kutumia haya maji na
ndio maana unaona wananchi wanafuraha nawameanza kunywa maji hapa hapa kwenye
kisima hiki kwa kuwa bado hawaamini kilichotokea”,walisema wananchi.
Wananchi wao wamemuomba
mbunge Ritta kabati na Diwani wa kata ya nduli Bashir Mtove kuendelea kutatua
changamoto za wananchi kwa kuwa walichaguliwa na wananchi kwa lengo la
kuwatumikia.
Kwa upande wake mbunge wa
viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM)
alisema kuwa wataendelea kutatua changamoto mbalimbali za wananchi kwa kuwa
yeye ni mbunge wa wananchi wote bila kubagua vyama.
Kabati alisema kuwa
ataendelea kuwachimbia visima na kukarabati majengo ya shule zilizochakaa
katika mkoa wa Iringa kwa kuwa yeye ni mbunge wa mkoa wa Iringa hivyo aliwaomba
wananchi kuendelea kuiamini serikali ya chama cha mapinduzi kwa kazi kubwa
wanayoifanya kupitia kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe
Magufuli.
“Hivi hamuoni nimeamua kufika huku ambako hata
viongozi wengi hawajafika ila mimi nimekuja nimewaleta kisima na maji safi na
nitaendelea kuja kutatua matatizo ya mtaa huu kwa kuwa tumetumwa na Rais
kufanya kazi kwa wananchi wa chini ndio maana hata mimi nimeanza kufanya kazi
huku mbali japo kuwa ndio jadi yangu kuwatumikia sana wananchi wa chini sasa
naombeni mniunge mkono katika juhudi zangu za kuwaletea mandeleo”.alisema
Kabati
Aidha Kabati alisema kuwa
lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuleta maendeleo kuanzia huku chini
kupanda juu hivyo tufanye kazi kwa kujituma ili tuende sambamba na kasi ya Rais
wetu.
Naye Diwani wa kata ya nduli
Bashir Mtove alimshukuru mbunge huyo kwa jihada zake za kuleta maendeleo na
kumuomba kushugulikia changamoto alizozitoa kwa wananchi ili kuendelea
kujijengea imani kwa wananchi wa kata hiyo.
Mtove aliongeza kuwa
atahakikisha kata yake inamaliza tatizo la maji ambao limetumu kwa miaka mingi
hivyo wananchi wanatakiwa kufanya kazi kwa kujituma ili kukuza uchumi wa kata
hiyo.
“Angalia hadi saizi
tumechimba visima zaidi ya sita kwenye kata yangu japo bado sana kumaliza
tatizo hili la maji hivyo naendelea kujituma kutafuta marafiki,wafadhili na
kumshirikisha mbunge Kabati kusaidia kutatua tatizo la maji na changamoto
nyingi ili wananchi wangu wafanye kazi kwa kujituma bila kuwa na vikwazo
vyovyote vile vya kiafya”.alisema Mtove.
No comments:
Post a Comment