ANGALIA LIVE NEWS

Friday, March 31, 2017

MIEZI MINNE BAADA YA UZINDUZI WA NDEGE MBILI ZA ATCL (BOMBARDIER), WAKUSANYA BILIONI TISA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la ATCL, Bw. Lasislaus Matindi anasema wamefanikiwa kukusanya Shilingi Bilioni 9 kwa Miezi minne tu kwa kutumia ndege hizo mbili zilizonunuliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, nakuleta utata mkubwa na wapinzani wa siasa nchini waliodai kuwa hazikuwa na tija kwa Taifa.
Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) ilianzishwa mwezi Novemba 2002 baada ya Serikali kubinafsisha lililokuwa Shirika la Ndege la Tanzania (Air Tanzania Corporation, ATC); katika Shirika hilo, Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) lilinunua hisa asilimia 49 ndani ya ATC. Hata hivyo ubia kati ya ATCL na SAA ulikabiliwa na matatizo ya kiuendeshaji na kulazimika kusitishwa mwezi Agosti 2006 na ATCL kurejeshwa tena Serikalini kwa asilimia 100.
KUMBUKUMBU:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na maafisa na viongozi wengine mbalimbali akikata utepe kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam Jumatano Septemba 28, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na maafisa wengine waandamizi wakiwa kwenye ndege mojawapo baada kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam Jumatano Septemba 28, 2016. PICHA NA IKULU.

1 comment:

Anonymous said...

Wale wapinzani wa siasa Tanzania wakiongozwa na Mbowe, Tundu Lisu na wenzake siku zote ni watu wenye mawazo ya hovyo ya kufikiria upizani ni kupinga kila kitu na hapana shaka mawazo yao ni ya kuirejesha nyuma nchi kimaendeleo baada ya kusonga mbele kama mueshimiwa raisi anavyopigania. Hata Zito Kabwe alieonekana mwanzoni ni mtu mweledi katika mambo mbali mbali lakini kila siku zinavyosonga mbele Zito Kabwe anaonekana kwanini chadema walimtimua yaani kawa mtu wa hovyo kabisa kwani amegeuka kuwa mtabiri yeye,mwanasiasa yeye,mchumi yeye,mwana habari yeye,wakili yeye,mdaku yeye amepoteza kabisa ile sifa yake ya kuwa mwanasiasa makini mwenye kutoa maoni yake ya kwa uangalifu. Mafanikio ya ndege mpya kimapato ndivyo itakavyokuwa katika miradi mengine mingi katika serikali ya magufuli. Maghufuli yupo serious lakini baadhi ya watanzania hasa wale walioshikiliwa akili zao na wapinzani wanaonekana kubeza hatua mbali mbali zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya tano katika kuiondoa Tanzania kutoka katika hali ya umasikini. Hata hizo habari njema za maendeleo ya shirika la ndege wao watakuja kubeza. Wakati umefika kwa watanzania wote kuamini yakwamba chini ya uongozi wa muheshimiwa Maghufuli watanzania tunaouwezo kuliondosha taifa letu kutoka hali ya umasikini tena katika kipindi kifupi. Siku watanzania tulikuwa tunalia na kuomba kumpata kiongozi makini wa kuliongoza taifa,kusimamia rasilimali zetu kwa uadilifu nakadhalika nakadhalika sasa kiongozi kapatikana hatutaki kumpa ushirikiano sasa huo kama si usaliti kwa Mungu kitu gani? Tunasahau yakwamba muomba kwenda peponi lazima afe kwanza. Hongera sana muheshimiwa raisi kwa uchapaji wa kazi iliotukuka watanzania weledi tunakuelewa na zamira zako njema kabisa Mungu atakulinda na maadui na atakupa maisha marefu,Amin.