Aliyewahi kuwa mwenyekiti
wa UVCCM,na Diwani wa Kata ya Sambasha mkoa wa Arusha Lengai Ole
Sabaya (aliyevaa suti nyeusi)akiwa nje ya mahakama mara
baada ya kuachiwa kwa dhamana kutokana na kesi inayomkabili.Picha na
Vero Ignatus Blog.
Aliyewahi kuwa mwenyekiti wa
UVCCM,na Diwani wa Kata ya Sambasha mkoa wa Arusha Lengai Ole
Sabaya (aliyevaa suti nyeusi)akizungumza na vyombo vya habari
nje ya mahakama.Picha na Vero Ignatus Blog.
Akizungumza na mwenyekiti wa CCM katika kata ya Sambasha Lesion Letionoki Njoki.Picha na Vero Ignatus Blog.
Akisalimiana na wananchi wa kata ya Sambasha mara
baada ya kuachiwa kwa dhamana.Picha na Vero Ignatus Blog.
Na Vero
Ignatus.Arusha
Mahakama
ya Hakimu mkazi Arusha imemsomea mashtaka mawili aliyewahi kuwa
Mwenyekiti wa umoja wa
vijana (UVCCM) Lengai Ole Sabaya ambaye pia ni diwani wa kata ya
Sambasha Wilaya ya Arusha vijijini .
Miongoni mwa makosa hayo
aliyosomewa mahakamani hapo kosa la kwanza alituhumiwa kujifanya Afisa
mtumishi wa serekali (TISS)huku kosa la pili ikiwa kugushi moja ya
nyaraka za serekali(kitambulisho ).
Akisoma mashtaka hayo
mahakamani hapo Wakili wa serekali Penina Joakim amesema kuwa Mnamo May
18 katika hotel ya Skyway iliopo makao mapya jijini Arusha Mshitakiwa
alijitambulisha kama Afisa utumishi wa idara ya usalama wa taifa na
kufanya Utapeli .
Wakili Penina alitaja kosa la pili ambalo
Mshitakiwa Lengai Ole Sabaya alisomewa kuwa ni kugushi kitambulisho cha
idara ya usalama wa Taifa kilichokuwa kikisomeka jamuhuri ya muungano wa
Tanzania idara ya usalama wa Taifa (TISS) Lengai Ole Sabaya kikosi
maalumu Agent (undercover)chenye code no MT 86117 huku akitambua kuwa ni
kinyume cha kisheria .
Hata hivyo mara baada ya kusomewa
mashtaka hayo mahakamani hapo mtuhumiwa alikana mashtaka ndipo Hakimu
Mkazi aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo Nestory Barro alisema dhamana
ipo wazi iwapo wathamini watakithi vigezo vinavyotakiwa na mahakama
hiyo.
Hata hivyo Mshitakiwa alipata dhamana baada ya kukithi
vigezo vilivyowekwa na mahakama ambapo ilikuwa ni wadhamini wawili wenye
sifa ambapo kwanza awe mtumishi wa serikali pili awe na mali
isiyohamishika yenye thamani ya shilingi milioni tatu kwa kila
mmoja.
Hata hivyo wakili Edina
Mndeme anayemtetea Lengai Ole Sabaya amesema kuwa mteja wake
amekuwa akifikishwa mahakamani na amesomewa mashitaka yaleyale na hii
ni mara ya nne .
Kesi
imeaihishwa na hakimu mkazi hadi itakapotajwa tena 30/8/2017 ambapo
uchunguzi unatarajiwa kukamilika na kesi hiyo kuanza
kusikilizwa.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake