Wednesday, August 9, 2017

Dk. Mpango atembelea banda la Benki ya Kilimo

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amelitembelea Banda la Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) wakati wa maonesho ya Nane Nane yanayofanyika kitaifa katika Viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.

Akiwa katika Banda hilo Dkt. Mpango alionekana kuridhishwa na jitihada za Benki ya Kilimo katika kuchagiza mapinduzi ya kilimo.

Akimpokea Waziri Dkt. Mpango, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Francis Assenga alimjulisha Dkt. Mpango kuwa ndani ya Banda la TADB jumla ya washiriki 14 wanaonesha bidhaa na huduma zao kupitia Benki hiyo ikiwemo wakinamama na vijana.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (aliyevaa fulana ya kijani) akiwasili kwenye Banda la Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) lililopo kwenye Viwanja vya Ngongo, mjini Lindi.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (kushoto) akikaribishwa kwenye Banda la TADB na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Francis Assenga (kulia).
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (kulia) akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea Banda la TADB. Anayemtazama ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Francis Assenga (kushoto).
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Francis Assenga (kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (katikati) mara alipotembelea Banda la Benki hiyo. Kulia ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bw. Simon Migangala.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (kulia) akizungumza na mmoja ya wanufaika wa mikopo ya TADB, Bibi Constancia Andrea (kushoto) kutoka Umoja Cashewnut Group.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (kulia) akizungumza na viongozi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), na Mfuko wa Kusaidia Kilimo (PASS) alipotembelea Banda la TADB. Wanaomsikiliza ni Mkurugenzi Mtendaji wa PASS, Bw. Nicomed M. Bohay (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (wapili kushoto). Wengine ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bw. Simon Migangala (katikati) na Meneja Mikopo wa TADB, Bw. Samuel Mshote (wapili kulia).

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake