Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kwa mara nyingine kesi ya kutakatisha fedha na kughushi inayowakabili Rais wa Simba SC, Evans Aveva na Makamu wake, Geofrey Nyange maarufu Kaburu hadi Agosti 22, 2017 baada ya upelelezi kutokamilika.
Kesi hiyo imeahirishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Mwambapa baada ya Wakili wa TAKUKURU, Kishenyi Mutalemwa kueleza kuwa upelelezi haujakamilika na kuomba iahirishwe hadi tarehe nyingine.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake