Friday, August 11, 2017

Misa ya Kiswahili, Jumapili August 13, 2017

Wakristu wapendwa,

Tumsifu Yesu Kristu.
Padre Peter Mushi na Padre Godfrey Amobi, wanapenda kuwatangazia ya kuwa,
Misa yetu ya kiswahili itafanyika Jumapili, tarehe 13 Mwezi Agosti, 2017, Saa 8:00 mchana (Sunday 13th August 2017 at 2 pm).

Tunawakaribisha watu wote wanaopenda kuhudhuria ibada yetu ya Kiswahili.

Anwani yetu ni: Kanisa la Mt. Cecilia, 120 East 106 Street, New York, NY 10029. Between Lexington and Park Avenue.

Chukua Train # 6. Mpaka kituo cha 110 St. Halafu tembea ukirudi mpaka 106 St.

Ni matumaini yetu kwamba mtafika kwa wingi. Karibuni sana tumshangilie Bwana, kwa lugha yetu ya Kiswahili.

Mbarikiwe.

Kutoka kwa Padre Peter Mushi na Padre Godfrey Amobi
Karibuni...sana..

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake