John Mwirigi.
Aliyekuwa mgombea wa Ubunge Igembe Kusini nchini Kenya, John Mwirigi (24) ameshinda nafasi hiyo baada ya matokeo kutangazwa na Tume huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).
Mwirigi ambaye anatajwa kuwa Mbunge mwenye umri mdogo kuwahi kutokea aliwashangaza wengi katika kampeni zake ambapo alikuwa akitumia baiskeli na bodaboda.
Mwirigi ambaye ni mwanafunzi wa Shahada ya elimu katika chuo cha Mount Kenya alikuwa mgombea binafsi hakuwahi kuwa na matangazo kwa kile kilichodaiwa kukosa pesa za kufanya kazi hiyo.
Katika matokeo hayo, Mwirigi alipata kura 18,867 huku mgombea wa Jubilee, Rufus Miriti akipata kura 15,411. GPL
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake