Simba Sports Club inataka kujenga ushirika mkubwa kabisa katika maeneo yote nchini kwa kushiriki katika matukio na shughuli mbalimbali za kijamii zinazolenga kurudisha kwa Jamii inayoizunguka kwa kuangalia maeneo yenye uhitaji ambapo viongozi,wachezaji, wanachama, wapenzi na mashabiki huungana kwa pamoja ili kutoa mchango wa hali na mali kwa Jamii yake kwani Simba ni Chapa (Brand) kubwa nchini na kwingineko Afrika na dunia kwa ujumla hivyo ushiriki wake kijamii una umuhimu mkubwa sana.
Simba Week itaadhimishwa kwa shughuli mbalimbali ikiwemo;
• Kutembelea watoto wanaofanyiwa upasuaji wa moyo
• Kugawa mipira kwenye kliniki
• Kampeni ya mtaa kwa mtaa
• Wachezaji kuongea na mashabiki
• Kukaribisha timu nyumbani
• Kupiga picha na kombe
Kikosi cha Simba ambacho sasa wameweka kambi mjini Johannesburg, Afrika Kusini, wanatarajia kucheza mchezo wao wa kwanza wa kirafiki leo dhidi ya Orlando Pirates katika maandalizi ya Simba Day Maandalizi ya Simba Day 2017 yanaendelea kupamba moto ambapo kauli mbiu ya Simba Day 2017 ni "KiSimba Zaidi".Tiketi za Simba Day zitaanza kuuzwa Agosti 4 ambapo watakao nunua kuanzai tarehe hiyo hadi Agosti 7 watapata punguzo la bei wakati watakaonunua Siku ya Simba Day watapata tiketi kwa bei ya juu zaidi. Hivyo tunawaomba wanachama, wapenzi na mashabiki wote wa Simba wanunue tiketi mapema kwa bei nafuu kabisa.
Simba wamesema kuwa taarifa zote rasmi kuhusiana na klabu zitaendelea kupatikana katika chanzo cha klabu (SIMBA APP), hivyo wanahabari wawe makini na tetesi za mitaani kwani mahali pekee pa uhakika pa kupata habari za Simba ni kupitia Simba App.
Afisa Habari Mkuu wa Simba, Haji Manara amesema kwamba kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali nchini watafanya mambo mengi ikiwemo yaliyoorodheshwa hapo awali.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group ambao ni wabia wa Simba kwenye masoko na biashara alisema "Simba Day na Wiki zimekuwa sherehe muhimu zikihusisha shughuli za kurudisha kwa Jamii na kuifanya Simba iwe karibu zaidi na wapenzi na mashabiki wake.
Simba inaamini katika kujenga chapa yake kupitia shughuli za kijamii na mikakati ya kimasoko na kuwa karibu na mashabiki na wapenzi wake
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake