Thursday, August 3, 2017

Washiriki kutoka Tanzania wa “Young African Leaders Initiative (YALI) 2017” watembelea Ubalozi wa Tanzania, Washington, D.C.

Tarehe 2, Agosti 2017) Wahiriki 42 wa Mandela Washington Fellowship 2017 kutoka Tanzania waliofika mwezi Juni, 2017, walitembelea Ubalozi wa Tanzania, Washington, D.C. na kukutana na Mheshimiwa Balozi Wilson M. Masilingi. YALI, ni programu iliyoanzishwa na Rais mstaafu wa Marekani Mheshimiwa Barack Obama kuwasaidia vijana wa Afrika kutembelea Vyuo vikuu vya Marekani kujifunza, kwa ufadhili wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani (U.S. Department of State). Baada ya kumaliza mafunzo katika vyuo mbalimbali Watanzania hawa walikuja Washington, D.C. kupokea vyeti na kutembelea Ubalozi wa Tanzania.
Mhe. Balozi Masilingi aliwaasa kuwa wazalendo, kupendana na kuwa waadilifu katika kuendeleza uchumi wa nchi yetu kwa kuanzisha na kukuza biashara. Aliwashauri pia kushirikiana na Ubalozi na Diaspora ya Watanzania waliopo Marekani, kukuza sekta ya utalii, biashara, elimu na ujenzi wa viwanda.

Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi akiwa na washiriki wa YALI Mandela Washington Fellows, 2017
Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi akiongea na Washiriki wa YALI, Mandela Wahington Fellows. (kulia) Afisa wa Ubalozi Bw. Dismas Assenga.

Yali Mandela Washington Fellows 2017 wakiongea na Mhe. Balozi.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake