Advertisements

Wednesday, March 21, 2018

58 WAKAMATWA OPERESHENI YA DAWA ZA KULEVYA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

JESHI LA POLISI TANZANIA


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MATOKEO YA OPERESHENI MAALUM ILIYOFANYIKA MJINI MAGHARIBI- ZANZIBAR, KUANZIA TAREHE 14 – 21.03.2018

Ndugu Wanahabari,

  1. UTANGULIZI ;
Zipo taarifa kuwa baadhi ya wananchi Mkoa wa Mjini Magharibi wanatumia, wanashiriki, wanafadhili au kusaidia biashara ya madawa ya kulevya kama ilivyo kwenye maeneo mengine nchini.

Hata hivyo Serikali ipo kwenye vita kali ya kupambana na mtandao wa madawa ya kulevya na Inspekta Jenerali wa Polisi kwa kushirikiana na Kamisheni ya Polisi Zanzibar waliunda timu kutoka Kitengo cha Operesheni Maalum za Polisi Makao Makuu Dar es salaam kuja kuongeza nguvu katika ufuatiliaji wa kero hii kama ilivyo kwenye maeneo mengine ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  1. MATOKEO YA OPERESHENI ;
S/N
MAFANIKIO
MATOKEO / IDADI
TAARIFA ZA INTELIJENSIA

Kupatikana kwa taarifa za  watuhumiwa wanaojihusisha na mtandao wa madawa ya kulevya (kutumia, kuuza, kufadhili au kusaidia)
105
JUMLA KUU
105

WATUHUMIWA  WALIOPATIKA NA HATUA

Watuhumiwa waliofikishwa Mahakamani
26

Watuhumiwa waliopo chini ya Upelelezi
16

Watuhumiwa waliopo chini ya uangalizi wa Polisi (Police Supervisee)
16
JUMLA KUU
58
VIELELEZO

Heroin  
Kete 1293 na Vifuko 3 sawa na
Gramu 74.385

Banghi (Vifurushi)
373

Banghi (Vifuko)
3


  1. WITO :
Natoa wito na tahadhari kwa wananchi wote wanaohusika kwenye mtandao huu kuacha mara moja kwa kuwa vita hii imeshaanza na inaendelea kwa lengo la kuhakikisha usalama wa vizazi vilivyopo na vizazi vijavyo maana madawa haya yanaathiri zaidi vijana ambao ndiyo muhimili na nguvu kazi ya Taifa.

Aidha nawapongeza wananchi wote waliotoa ushirikiano wa kutoa taarifa za uhalifu huu bila ya kuona muhali. Niwaombe wananchi wote kuendelea na ushirikiano huu wa kutoa taarifa.

Mwisho natuma salamu kwa watuhumiwa wote waliotoroka kule walipo wajue kuwa wanatafutwa na watakamatwa ili wahojiwe na hatimae kufikishwa Mahakamani.

Ahsanteni sana kwa kunisikiliza

Liberatus Sabas – DCP
Mkuu Wa Uperesheni Maalum za Polisi Tanzania

21.03.2018

No comments: