ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, May 31, 2018

Taarifa Ya Msiba - Springfield, MA


TANZIA

Kwa masikitiko makubwa tunasikitika, tunawatangazia kwamba mmoja wa UMOJA Church Prayer Line Managers Bi Aida Mwangata wa Springfield, MA amefiwa na mchumba wake Mr. Josiah CHACHA Jumanne May 29, 2018. 

Mipango ya kumsafirisha marehemu, mchumba wake na Mama Mzazi wa marehemu imeshaanza pale Boston, MA kwenda kwenye mazishi Dar Es Salaam, TZ imeanza. 


Marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa tumbo (yaani Gallstone) pamoja na Pheumonia. Hali yake ilibadilika ghafla weekend hii ambapo pressure yake ilishuka mno na kuleta mauti yake kufikia J'nne. 

Kwa taarifa zaidi: 

Unaweza wasiliana moja kwa moja na:
Aida (Fiancee) : 413-693-5432
Sada (Dada wa marehemu): 413-204-1321
Richard Mwandemani: 413-262-0400

Msiba upo nyumbani kwa marehemu:

540 Grandy Rd
South Hardley, MA 01075

Kwa Rambirambi

Kuisindikiza familia hii kwa rambirambi, tafadhali tumia njia yeyote kati ya hizi:

*CashApp*

Aida Mwangaka: 413-693-5432
Amina Makoko : 413-204-1321

*GoFundMe*

Bank Account
Bank of America (BOA)
Acct : *004648822691*
Routing: *011000136*
Name: Veronica Bisege

BWANA Ametoa, BWANA Ametwaa, Jina lake lihimidiwe. 

AMEN. 

*UONGOZI, UMOJA CHURCH*
Kwa niaba ya familia.

Serikali Kuendelea Kuchukua Hatua za Kisera Kuhakikisha Riba za Mikopo Zinapungua

Waziri wa Madini Mhe. Angellah   Kairuki akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Fedha ya Wizara hiyo kwa mwaka 2018/2019 leo Bungeni  Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Uratibu  Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akitoa maelezo  Bungeni kuhusu hatua zitakazochukuliwa na Serikali katika kuwalinda watoto wa kike ambapo ameahidi kuwa Serikali itatoa taarifa rasmi kuhusu kuwepo kwa baadhi ya watu wanaowadhalilisha kijinsia watoto wa kike  na hatua zilizochukuliwa na Serikali.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza kuhusu mikakati ya Serikali kupambana na Janga la Ukimwi hapa nchini ikiwemo kuhamasisha upimaji wa Virusi vya UKIMWI  hasa kwa wanaume kote nchini ili wajue hali zao na kuchukua hatua stahiki.

Serikali Yatoa Milioni 700 kwa vijana mwaka 2017/18


 Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana - ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Juma Abubakari (aliyesimama mbele) akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha Jukwaa la Vijana Kitaifa cha vijana waliowezeshwa Kiuchumi kupitia mradi wa YEE unaofadhiliwa na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) na kutekelezwa na Shirika la Plan International – Tanzania.
 Mwenyekiti wa Jukwaa la vijana walionufaika na mradi wa YEE, Mwajuma Chamkono akichangia hoja wakati wa kikao cha Jukwaa la Vijana Kitaifa cha vijana waliowezeshwa Kiuchumi kupitia mradi huo unaofadhiliwa na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) na kutekelezwa na Shirika la Plan International – Tanzania.

WIZARA, TAASISI ZA SERIKALI ZITUMIE NISHATI MBADALA – WAZIRI MKUU

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati alipowasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja kuzindua Maadhisho ya Wiki ya Mazingira, Mei 31, 2018. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Dar es salaam, Kate Kamba wakati alipowasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam kuzindua Wiki ya Mazingira, Mei 31, 2018. Wapili kushoto ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla na watatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani , Mhandisi Evarest Ndikilo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Space Engineering Limited, Bw. Philip Mtui kuhusu mkaa uliotengenezwa kutokana na takataka na kufungashwa kwenye kiroba tayari kwa kuuzwa wakati alipotembelea banda la Kampuni hiyo kabla ya kuzindua Wiki ya Mazingira kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei 31, 2018. katikati ni Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi, Evarest Ndikilo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuuu)

Reli ya Kisasa itakuwa na Daraja lenye urefu wa Km 2 8


TBL GROUP YAADHIMISHA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI KWA KUPANDA MITI MKOANI KILIMANJARO

 Wafanyakazi wakijiandaa kuanza zoezi la kupanda miti wilayani Siha, Kilimanjaro.
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL waliopo katika mafunzo ya kukuza vipaji wakishiriki zoezi la kupanda mito wilayani Siha, Kilimanjaro.

UNESCO TO SUPPORT ONE MONTH ANTI FGM CAMPAIGN IN 5 REGIONS

UNESCO is supporting the organization of a one-month anti-FGM campaign in selected districts within the five regions with high prevalence namely Manyara, Dodoma, Arusha, Mara and Singida. The campaign is organized with financial support from SDC project, Sida O3 Project and UNDAP II- VAWC One UN fund. 
The campaign kicked off in Ngorongoro on May 28 and will include a 3-day capacity-building workshop to be conducted in collaboration with Loliondo FM, a UNESCO supported community radio, followed by official launch of the campaign on 31st May and an intergeneration dialogue on ending FGM practices and traditional to be aired live by Loliondo FM. 
The workshop is meant to orient key anti-FGM campaigners including media practitioners with key messages where a major public campaign through five community radios within the top five regions will be carried out there after expected to reach 1 million people. 
Community radios for the public campaign with regions in brackets include Loliondo FM (Arusha), ORS (Manyara), Dodoma FM (Dodoma will also cover Singida), Triple A FM (Arusha), Mazingira FM (Mara). 
The key approaches for the Ngorongoro anti-FGM campaign include a Public Campaign through Community Radios highlighted where a series of community radio sessions will be developed and broadcasted targeting community leaders, law enforcers, medical personnel, religious leaders, Ngaribas and young people (particularly out of school girls. 
The other approach will involve a School-based campaign, specifically targeting pupils, students, 
teachers, and school-parent committees from 20 schools in Loliondo division.. 

Kesi ya Bilionea Msuya: Wazee Wataka Washitakiwa Wote Waachiwe Huru

Maoni ya mzee mshauri wa mahakama katika kesi ya mauaji ya kukusudia ya bilionea Erasto Msuya, Herry Msangi jana yalimfanya dada wa marehemu, Antuja Msuya kuangua kilio mahakamani.

Wakitoa maoni yao mbele ya Jaji Salma Maghimbi anayesikiliza kesi hiyo, Msangi na mwenzake, Marry John waliiomba mahakama iwaone washtakiwa wote hawana hatia na iwaachie huru.

Hata hivyo wakati akiahirisha kesi hiyo, Jaji Maghimbi alisema amesikia maoni ya wazee hao na kwamba yatatiliwa maanani, lakini hayaifungi mahakama katika uamuzi wake.

Kabla ya kuahirisha kesi hiyo hadi hapo itakapotolewa notisi ya tarehe ya kusomwa kwa hukumu, Jaji Maghimbi aliwataka mawakili wa pande zote mbili kukutana naye kwa faragha katika chemba yake.

Mawakili hao ni wa Serikali, Tamari Mndeme na Ignasi Mwinuka na wale wa utetezi ambao ni Hudson Ndusyepo, Majura Magafu, Emmanuel Safari na John Lundu.

Msangi ndiye aliyekuwa wa kwanza kutoa maoni yake kwa muda wa saa 1:40 kuanzia saa 4:30 asubuhi hadi saa 6:10 mchana na kufuatiwa na Marry aliyetoa kwa dakika tano kuanzia saa 6:20 mchana.

Mara tu alipomaliza kutoa maoni yake hayo, dada wa marehemu alianza kuangua kilio kwa sauti ya juu huku akitoka kortini, na alipotoka hatua tatu kutoka mlangoni aliongeza sauti.

Mahakama Kenya Yazuia Vifungu 26 Sheria ya Makosa ya Mtandaoni

Mahakama Kuu ya nchini Kenya imezuia matumizi ya vifungu kadhaa vya Sheria ya mtandao iliyopitishwa na kusainiwa na Rais Kenyatta wiki mbili zilizopita nchini humo.

Mahakama imevizuia vifungu 26 vya Sheria hiyo mpaka hapo shauri litakaposikilizwa, hatua hii inafikiwa baada vya chama cha Wanahabari na waendeshaji wa Blogu kufungua pingamizi.

Akitoa uamuzi huo Jaji wa Mahakama Kuu, Chacha Mwita amesema kuwa sheria hiyo ni kandamizi kwa haki za binadamu ikiwemo uhuru wa kujieleza.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 18 mwaka huu ambapo itasikilizwa tena.

Zungu Aitaka NHC Iache Kupandisha Kodi Kiholela

Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mussa Azzan Zungu, amelitaka Shirika la nyumba la Taifa (NHC) kuacha tabia ya kuongeza kodi mara kwa mara kwa wananchi ambao ni wapangaji katika nyumba hizo.

Zungu amesema hayo jana Mei 30, 2018 Bungeni Jijini Dodoma, baaada ya kupitishwa kwa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi kwa mwaka wa fedha 2018/2019 na kuongeza kuwa wapangaji katika nyumba hizo wengi ni maskini hawana uwezo wa kulipa kodi zinazopanda kila kukicha.

“Mkurugenzi wa shirika la nyumba, maagizo ya Waziri Mkuu umeyasikia, kaa na kamati ya wapangaji, mimi shida kwangu ni nyumba ndiyo ajenda zangu za Ubunge na Waziri Mkuu amesema muachane na haya mambo ya kupandisha kodi kiholela, hawa ni watanzania hawana uwezo huo” alisema Zungu

Kwa upande mwingine mwenyekiti huyo aliipongeza Wizara hiyo kwa kuleta mabadiriko ya kiutendaji na kusaidia kupunguza migogoro ya ardhi nchini.

Huu hapa Wimbo wa Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo Wote


Balozi Seif afanya mazungumzo na Balozi wa Jamuhuri ya Cuba

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kulia akisalimiana na Balozi wa Jamuhuri ya Cuba Nchini Tanzania Profesa Lucas Domingo alipofika kwenye Makaazi yake Jijini Dar es salaam kumpongeza kwa Cuba kumaliza Uchaguzi wa Rais salama.
Balozi Seif akitia saini Kitabu cha Wageni mara baada ya kukaribishwa kwenye Ubalozi wa Jamuhuri ya Cuba Nchini Tanzania Jijini  Dar es salaam.

Mkutano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji wafikiatamati

Mhe. Mhandisi Stella Manyanya Naibu Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji akifuatilia Mkutano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji la Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea.

Mkutano huu ulilenga kujadili na kutolea ufumbuzi masuala mbalimbali yakiwemo ya kiforodha, ambayo yamekuwa kikwazo katika ufanyaji wa biashara za kuvuka mipaka katika Jumuiya.

Mkutano huu uliofanyika kuanzia tarehe 25 hadi 30 Mei, 2018 na kuhudhuriwa na nchi zote wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki ulifikia tamati tarehe 30 Mei, 2018 jijini Arusha.
Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akizungumza kwenye Mkutano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji uliofanyika jijini Arusha.

Wednesday, May 30, 2018

UJumbe wa Saudi Arabia wakutana na Dk.Shein

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na  Waziri wa Mamlaka ya Saudi Arabia anayeshuhulikia Mambo ya Kiislamu, Misaada, Daawa na Miongozo Mhe. Dk.Sheikh Saleh bin Abdul Aziz bin Muhammad bin Ibrahim Al Sheikh, akifuatana na Ujumbe wake walipofika Ikulu Mjini Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akizungumza na Waziri wa Mamlaka ya Saudi Arabia  anayeshuhulikia Mambo ya Kiislamu, Misaada, Daawa,na Miongozo Mhe,Dk.Sheikh Saleh bin Abdul Aziz bin Muhammad bin Ibrahim Al Sheikh,(wa tatu kulia)  alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akifuatana na Ujumbe wake.

DKT. ASHATU KIJAJI AZIPONGEZA BENKI KUSHUSHA RIBA ZA MIKOPO

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akifunga  warsha ya wadau wa Sekta ya Fedha iliyolenga kujadili mchango wa sekta hiyo katika kukuza uchumi wa viwanda leo Jijini Dodoma.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatib Kazungu akizungumza wakati wa  kufunga warsha  ya wadau wa Sekta ya Fedha iliyolenga kujadili mchango wa sekta hiyo katika kukuza uchumi wa viwanda leo Jijini Dodoma. 
 Mbunge wa Jango’mbe Mhe. Ally Hassan King akizungumza  wakati wa  kufunga warsha ya wadau wa Sekta ya Fedha iliyolenga kujadili mchango wa sekta hiyo katika kukuza uchumi wa viwanda leo Jijini Dodoma.

YALIYOJIRI LEO BUNGENI JIJINI DODOMA

 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Kangi Lugola akijibu swali kuhusu utaratibu unaotumika kutoa ajira kwa wananchi katika sekta za Muungano leo Bungeni Jijini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Madini Mhe. Stanslaus Nyongo akisisitiza jambo kwa Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki  na Naibu Waziri Mhe. Dotto Biteko leo Bungeni  Jijini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali  na majibu.
 Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Tate Ole Nasha akieleza mikakati ya Serikali kuhakikisha kuwa inajenga vyuo vya ufundi stadi kila Wilaya hapa nchini leo  Bungeni  Jijini Dodoma.

RAIS MAGUFULI ALIPOPOKEA RIPOTI YA UHAKIKI WA MALI ZA CCM, KATIBU MKUU MPYA WA CCM ALIPOTANGAZWA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Visiwani) Dkt. Ali Mohamed Shein wakiwa na 'mlima' wa makabrasha ya ripoti ya uhakiki wa mali za chama baada ya kukabidhiwa na tume aliyounda kuchunguza mali hizo ukumbi wa Kikwete jijini Dar es salaam Mei 29, 2018
 Wa kwanza kushoto ni Dkt Bashiru Ali Kakurwa ni Mwenyekiti wa Tume iliyoundwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt John Pombe Magufuli kuchunguza na kuhakiki mali za CCM akiwa na wajumbe wa tume hiyo mara tu baada ya jina lake kupendekezwa kuchukua nafasi ya Katibu Mkuu wa CCM mbele ya wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho ukumbi wa Kikwete jijini Dar es salaam Mei 29, 2018

WAZIRI MKUU MAJALIWA AZINDUA MAADHIMISHO YA MIAKA 15 TANGU KUANZISHWA KWA MFUKO WA DHARURA WA RAIS WA MAREKANI WA KUPAMBANA NA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI (PEPFAR)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Maadhimisho ya Miaka 15 Tangu Kuanzishwa kwa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na Kudhibiti Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (PEPFAR) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Mei 30, 2018.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza katika Uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 15 Tangu Kuanzishwa kwa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na Kudhibiti Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (PEPFAR) kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Mei 30, 2018.Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Katibu Tawala Morogoro awataka Maafisa Kilimo kuongeza Uzalishaji

Na Andrew Chimesela – Morogoro

Maafisa Kilimo wa Sekretarieti ya Mkoa na Halmashauri za Mkoa wa Morogoro wametakiwa kusimamia na kutoa utalaama wao kwa wakulima kupitia maafisa Ugani ili kuongeza uzalishaji wa mazao Mkoani humo.
Agizo hilo limetolewa Mei 29 mwaka huu na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bw. Clifford Tandari alipofanya Kikao na Maafisa wa Kilimo huo kilicholenga kupokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli za kilimo za kila Halmashauri na kuweka mikakati ya kuongeza uzalishaji kwa mwaka 2018/2019.
Akifungua Kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bw. Tandaria amesema, kila Afisa kilimo ahakikishe anasimamia Maafisa Ugani wake kwenda kwa wakulima kuwafundisha kilimo cha kisasa kwa kuwa wengi wao bado wanalima kilimo cha mazoea jambo linalowakosesha tija katika kilimo.
“sio wakulima waendelee na utaratibu ule ule wa zamani, tuhakikishe wakulima tunaweleza mbegu mpya zilizojitokeza na kuwasimamia kufanya palizi kwa wakati alisema ” alisema Tandari
Tandari amesema endapo watajipanga vizuri katika kuwasimamia Maafisa Ugani kuwafundisha wakulima kilimo cha kisasa na kuondoa kabisa upotevu wa mazao yanayopotea wakati wa kuvuna, upo uhakika wa kuongeza uzalisha wa mazao mara mbili ya matarajio ya mavuno ya mwaka huu ya kupata tani 2,800,000 katika Mkoa.

MAKAMU WA RAIS AFUTARISHA TUNGUU ZANZIBAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Rais wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi mara baada ya kufutari kwenye Makazi ya Makamu wa Rais, Tunguu Zanzibar jana jioni tarehe 29 Mei 2018.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Balozi Mdogo wa Ujerumani nchini  Mhe. Jens Dominic Warth mara baada ya kufutari kwenye Makazi ya Makamu wa Rais, Tunguu Zanzibar jana jioni tarehe 29 Mei 2018. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Mamoudou Gassama: 'Spiderman' aliyeishangaza Ufaransa kwa kumuokoa mtoto kutoka kwenye jengo la ghorofa apewa uraia


Mhamiaji wa Mali amepongezwa kama shujaa baada ya kukwea sehemu ya mbele ya jengo la ghorofa mjini Paris kumuokoa mtoto aliekuwa kwenye uzio wa ubaraza wa ghorofa ya nne kwenye jengo refu.

Video ya Mamoudou Gassam akimuokoa mtoto ilisambaa sana kwenye mitandao ya kijamii.

Alivuka kutoka kwenye ubaraza mmoja hadi mwingine kwa muda wa chini ya dakika moja akamvuta mtoto huyo aliyekuwa amekwama na kumsalimisha.


Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron baadaya kukutana na Bw Gassama kwenye makazi yake ya Elysee Palace Jumatatu kumshkuru binafsi alitangaza kumpa uraia wa taifa hilo.

Alimpa pia medali ya ushujaa na kumuahidi nafasi ya kazi katika idara ya zima moto

Meya wa Paris Anne Hidalgo pia alisifu sana ushujaa wa mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 22, na akasema alimpigia simu kumshukuru.

Alimuelezea kama "Spiderman wa 18", akimaanisha wilaya nambari 18 ambako uokoaji huo ulifanyika mjini Paris.

TSC yaonya walimu wanaodanganya umri wa kustaafu

Katibu, Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Walimu, Bibi Winifrida Rutahindurwa akiongea na walimu wakuu na wakuu wa shule (hawapo pichani) kutoka Wilaya za Bagamoyo na Chalinze. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bagamoyo, Bibi Fatuma Latu, wa kwanza kulia ni Katibu Msaidizi Tume ya Utumishi wa Walimu Wilaya ya Bagamoyo, Bibi Happy Kabuka akifuatiwa na Katibu Tawala wilaya ya Bagamoyo Bibi, Erica Yegela.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo Bibi, Erica Yegela akiongea katika mkutano wa walimu wakuu na wakuu washule mjini Bagamoyo. Wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bagamoyo, Bibi Fatuma Latu (wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Katibu, Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Walimu, Bibi Winifrida Rutahindurwa pamoja na maofisa wengine walioambatana nao.

FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY WATOA SOMO KUELEKEA UCHAGUZI NCHINI

a
Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society Bw. Francis Kiwanga akitoa ufafanuzi mbele ya wageni waalikwa mapema leo jijini Dar es salaam wakati akifungua  mkutano wa kujadili nafasi ya Asasi za kiraia katika chaguzi zijazo hapa nchini.

Asasi za kiraia nchini zimetakiwa kujitoa katika kuhakikisha wananchi wanashiriki kwa wingi katika chaguzi mbalimbali ikiwemo ya serikali za mitaa na wa serikali kuu wa mwaka 2020.

Hayo yamesemwa mapema leo Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society Bw. Francis Kiwanga alipokuwa akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi, wenye lengo la kujadili hali ilivyo kabla ya kufikia uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika hapo mwakani.

Mzee Gallus Abeid kutoka Mwalimu Nyerere Foundation akichangia mjadala mapema leo jijini Dar es salaam katika Mkutano wa Uchaguzi ulioandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali la Foundation for Civil Society.

MKANDARASI WA KITUO CHA AFYA GAIRO ATAKIWA KUMALIZA KAZI KWA WAKATI


 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (aliyeshika tofali na mwiko) na Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (mwenye blauzi nyekundu) pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Rachel Nyangasi (wa kwanza kulia) wakishirikiana kujenga ukuta wa Kituo cha Afya cha Halmashauri ya Wilaya ya Gairo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo aliyoifanya mwishoni mwa wiki iliyopita.

Tuesday, May 29, 2018

DKT. BASHIRU ALLY APITISHWA NA NEC KUWA KATIBU MKUU WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally akizungumza na wajumbe wa mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa NEC wakati akiwasilisha Ripoti ya Uhakiki wa mali za Chama cha Mapinduzi CCM kwa wajumbe hao Ikulu jijini Dar es Salaam
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiimba pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM-Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya kukabidhiwa makabrasha yenye taarifa za uhakiki wa mali za Chama hicho.

SEKTA YA FEDHA YATAKIWA KUONGEZA UBUNIFU KATIKA UTOAJI WA MIKOPO


 Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Maria Kangoye (kushoto) akizungumza jambo wakati wa mkutano kati ya  wadau wa sekta ya Fedha na Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.
 Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Florens Luoga (katikati), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu (kulia), na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Prof. Faustin Kamuzora (kushoto), wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya Fedha na Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei, akisikiliza kwa makini wito wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Florens Luoga (hayupo pichani) kuhusu Sekta ndogo ya Benki kuongeza ubunifu kwa kutoa mikopo ya muda mfupi na mrefu ambayo itawezesha ukuaji wa sekta za viwanda, Jijini Dodoma.

Tanzania itaendelea kushiriki katika ulinzi wa amani duniani, Balozi Mahiga

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akihutubia katika maadhimisho ya miaka 70 ya Siku ya Walinda Amani Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Mashujaa vya Mnanzi Mmoja Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Mei 2018. 

Siku ya Walinda Amani Duniani huadhimishwa tarehe 29 Mei ya kila mwaka ambapo kaulimbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni "Ulinzi wa Amani wa Umoja wa Mataifa: Miaka 70 ya huduma na kujitoa (UN Peacekeeping: 70 Years of Service and Sacrifice).

Katika hotuba yake, Mhe. Waziri Mahiga alieleza kuwa yapata miaka 12 tangu Tanzania ianze kushiriki katika ulinzi wa amani chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa. 

Pia akasisitiza Tanzania itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha inasaidia kupatikana kwa amani katika mataifa mengine kwakuwa hakuna taifa linaloweza kufanikiwa katika maendeleo pasipo kuwepo na amani ya uhakika. " Sio jambo rahisi kukubali kutoa uhai wako kwa ajili ya mtu mwingine lakini Tanzania itaendelea kuungana na mataifa mengine duniani katika kusaidia kupatikana kwa amani ya mataifa hayo" alisema Mhe. Mahiga.

Aidha, Katika kuwakumbuka Walinda Amani wote Duniani waliopoteza maisha wakati wakitekeleza majukumu yao, pamoja na kutoa heshima kwa wale ambao bado wanaendelea na jukumu la kulinda amani, Tanzania imepoteza jumla ya askari wapatao 30 ndani ya miaka 10, pia dunia imepoteza zaidi ya askari 3500 na kwa sasa Tanzania inajivunia kuwa na jumla ya askari wapatao 2,600 wanaohudumu katika misheni sita (6) za ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa.

Khadija Kopa : Wasanii Wengi Wamekuwa Jeuri, Muda Si Mrefu na Mimi Ntaacha Muziki

Msanii mkongwe wa taaarabu nchini Khadija Kopa amefunguka na kuzungumzia hali ya taarabu ilivyo sasa nchini na kusema kuwa wasanii wengi wamekuwa jeuri na kwamba hawajitunzi kama zamani hivyio wanajishusha thamani wao wenyewe na wala sio kitu kingine. 

Khadija kopa anasema kuwa wasanii wa taarabu wamekuwa wakiimba katika ma bar kwa kiinglio cha bia wakati hiyo haikuwa kama zamani na ili kukomesha hilo waimbaji hao wanatakiwa wakifuatwa wasikubali kufanya hivyo  na kujiona wa thamani ili kupanda hadhi yao.

Hata hivyo akizungumzia swala la yeye kustaafu kama alivyofanya gwiji wa taarabu nchini, mzee Yusup, malkia huyo amesema kuwa alichokifanya mzee ni kutokana na imani yake ilivyomtuma na ni jambo zuri , hata yeye siku yoyote atastaafu na sio muda mrefu kutoka sasa kwa sababu anahitaji kutenga muda mwingi pia kwa ajili yake , dini na mungu wake kwa sababu hajuai siku wala saa ya kufa kwake.

Hata hivyo Khadija Kopa anasema kuwa kama ataamua kufanya hivyo atafanya kimya kimya bila kumwambia wala kutangaza kwa watu, bali watashangaa tu haingii tena studio wala haonekani tena katika maswala ya burudani.

"Sina muda mrefu sana nitaacha huu muziki na nitakapo acha wala sina haja ya kutangaza eti eeh ninaacha muziki, hapana  nitaacha tu na watu wataona kimya tu sitoi nyimbo."