Advertisements

Monday, October 8, 2018

MTANGAZAJI NGULI WA RTD NA TBC MAREHEMU AHMED JONGO AZIKWA JIJINI DAR ES SALAAM LEO


 Maziko ya Mtangazaji wa RTD Ahmed Jongo  yamefanyika leo  makaburi ya Mbagala Charambee Dar es Salaam
 Mtangazaji mkongwe na mmiliki wa redio ya Sports FM Abdallah Idrisa Majura akijumuika na ndugu, Jamaa na marafiki kupata chakula nyumbani kwa marehemu Tandika Maghorofani leo mchana kwenye mazishi ya aliyekuwa Mtangazaji mkongwe wa Radio Tanzania (RTD),Ahmed Jongo.
 Sehemu ya waombolezaji wakiwamo ndugu, jamaa na marafiki wakijadiliana jambo nyumbani kwa marehemu aliyekuwa mtangazaji nguli wa  Radio Tanzania (RTD),Ahmed Jongo, nyumbani kwake Tandika Maghorofani,jijini Dar es Salaam, wakiwemo wacheza kandanda nyota wa zamani akiwemo (kutoka kulia) Suleiman Mkati, Kaburu, Mohamed Hussein Mmachinga pamoja na mafundi mitambo wa toka enzi za RTD Mzee Ali Saidi Tunku na Juma Kengele
  Miongoni mwa ndugu, jamaa na marafiki wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa nyumbani kwa aliyekuwa Mtangazaji mkongwe wa Radio Tanzania (RTD),Ahmed Jongo Tandika Maghorofani ambaye amefarikia dunia jana. Kutoka kulia ni mwanamuziki mkongwe Waziri Ally wa Njenje (zamani Msondo Ngoma) fundi mitambo James Mhillu, Adam Gille na Ankal.
 Watangazaji, mafundi mitambo wacheza kandanda nyoya wa enzi hizo na viongozi wa soka wakipata picha ya kumbukumbu baada ya kujumuika na   ndugu, jamaa na marafiki  nyumbani kwa marehemu aliyekuwa Mtangazaji mkongwe wa Radio Tanzania (RTD),Ahmed Jongo  Tandika Maghorofani,jijini Dar es Salaam.
Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

No comments: