ANGALIA LIVE NEWS

Friday, May 31, 2019

KAMPUNI YA GREEN WASTE PRO YAWEKA MAPIPA YA KUKUSANYIA MIFUKO YA PLASTIKI KWENYE MIJI YA DAR,DODOMA NA MWANZA


 Meneja wa Green Waste Pro tawi la Dodoma, Abdalla Mbena akizungumza katika tukio.


KAMPUNI ya Green Waste Pro (GWP)  kwa kushirikiana na Halmashauri za Miji ikiwemo ya Dar es Salaam, Dodoma na Mwanza  wamekuja na mkakati maalum ya kukusanya mifuko ya plastiki katika kuunga mkono juhudi za Serikali kutokomeza matumizi ya mifuko zoezi lililoanza toka Mei 25, mwaka huu.
  
Akizungumza Meneja wa Green Waste Pro tawi la Dodoma, Abdalla Mbena  katika mkutano uliandaliwa na Shirika la ForumCC kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam  ambapo amebainisha kuwa,  tayari wamesambaza mapipa zaidi 60 kwenye miji ya Dodoma, Mwanza na Dar es aSalaam katika Manispaa ya Ilala.
 
“Kwa kuunga juhudiz zoezi la kutokomeza mifuko ya plastiki ‘rambo’ sisi kama Green Waste Pro, tumeweza kusambaza mapipa hayo karibu kila eneo tulilotenga na wananchi wataweza kukusanya mifuko hiyo hapo.

Ili kuweka mazingira rahisi ya kutekeleza agizo hilo la Serikali la katazo la matumizi ya mifuko hiyo zoezi litakaloanza Juni Mosi mwaka huu.” Alisema Mbena.

Mbena ameonegza kuwa, wananchi wametakiwa kupeleka mifuko hiyo kwenye vituo hivyo  vya kukusanyia pamoja na maeneo mengine yaliyotengwa na Serikali.

Green Waste Pro wameweka mapipa hayo kwa Halmashauri Ilala katikati  eneo la Kaburi moja Mitaa ya Samora, Jamhuri na Libya huku pia wakiweka katika maeneo mengine ya katikati katika miji ya Dodoma na Mwanza.
 
Mwisho Mbena amewataka wananchi kuchangamkia nafasi hiyo na kuiwakilisha mifuko hiyo kabla ya kuanza kutozwa faini.

Katika tukio wamewakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wakandarasi wa kubeba taka ngumu kwa lengo la kujadili changamoto za kimazingira na kutafuta ufumbuzi wake.

Mjadala huo unafanyika chini ya ufadhili wa Umoja wa Ulaya(EU) kupitia Mradi wa Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi.
EU wamekuwa wakishirikiana kuandaa mijadala na makongamano yanayohusu kujadili mabadiliko ya tabianchini na hali ya mazingira nchini kwa ujumla.

Awali akizungumza wakati wa ufunguzi wa  majadiliano kwa niaba ya Meya wa Ilala, Naibu Meya wa manispaa hiyo Omari Kumbilamoto alisema ni jambo muhimu wadau kukutana na kuweka mikakati itakayosaidia kuweka mazingira safi hasa kwa kuzingatia Serikali imetangaza kuanzia Juni 1,mwaka huu ni marufuku kwa mtu yoyote kuzalisha, kuingia au kutumia mifuko ya plastiki.

Alisema Ilala ni ndio inayobeba taswira ya nchi na hivyo lazma izingatie kwamba inalo jukumu la kuweka mikakati kwa kushirikiana na wadau wa mazingira kuweka mazingira safi yakiwamo ya kuondoa taka ngumu

Mwandishi wa Habari  hii ni Mjumbe wa Bodi ya Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira (JET),

WAZIRI MKUU AMWAKILISHA RAIS MAGUFULI KATIKA SHEREHE ZA KUMWAPISHA RAIS WA MALAWI PROFESA ARTHUR MUTHARIKA

 Waziri Mkuu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na , Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Malawi, Ben Botolo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Chileka uliopo Blantyre Malawi kumwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika sherehe za kumwapisha Rais wa Malawi, Profesa  Arthur Peter Mutharika, Mei 31, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Malawi,  Bw. Ben Botolo wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Chileka uliopo Blantyre nchini Malawi kuwakilisha, Rais Dkt John Pombe Magufuli katika sherehe za kumwapisha Rais wa Malawi, Profesa, Arthur Peter Mutharika, Mei 31, 2019. 

Save the date! - Announcing the 2019 DICOTA Health Forum in Washington, DC


Please save the date,

 Saturday November 9th, 2019, Washington, DC area.

Join us for this unique and informative one day session to discuss healthcare in Tanzania.
#DICOTAHealth



Thursday, May 30, 2019

Save the date! - Announcing the 2019 DICOTA Health Forum in Washington, DC


Please save the date!
 Saturday November 9th, 2019, Washington, DC area.
Join us for this unique and informative one day session to discuss healthcare in Tanzania.


WIZARA YA MAMBO YA NJE YAWASILISHA BAJETI BUNGENI LEO

Baadhi ya Mabalozi wanaoziwakilisha Nchi zao hapa Nchini Tanzania wakifuatilia uwasilishaji wa hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki iliyowasilishwa na Waziri Profesa Palamagamba John Kabudi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. May 30, 2019
Baadhi ya Wakurugenzi na Wakuu wa Idara wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia uwasilishaji wa hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo iliyowasilishwa na Waziri Profesa Palamagamba John Kabudi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. May 30, 2019

RAIS DKT MAGUFULI AREJEA NCHINI AKITOKEA AFRIKA KUSINI, NAMIBIA NA ZIMBABWE

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Brigedia Jenerali Abdallah M. Alphonce na wafanyakazi wa ubalozi huo Bi. Alice Madele na Bi Joyce Makoye katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Robert Mugabe jijini Harare, kabla ya kupanda ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kurejea nyumbani akitokea Afrika Kusini alikohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuelekea nchini Namibia na Zimbabwe ambako alifanya ziara rasmi ya siku mbili kwa kila nchi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitelemka kutoka katika ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Alhamisi Mei 30, 2019 akitokea Afrika Kusini alikohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuelekea nchini Namibia na Zimbabwe ambako alifanya ziara rasmi ya siku mbili kwa kila nchi.

KAMATI YA MIUNDOMBINU YAFANYA TATHIMINI YA UKAGUZI WA MIRADI

 Katibu wa Kamati ya Miundombinu,Hosiana John akisoma taarifa ya tathimini ya utekelezaji wa ziara za kukagua miradi zilizofanywa na Kamati hiyo katika kipindi cha mwaka 2018/2019 kkwenye kikao cha kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Moshi Kakoso akizungumza katika kikao cha kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma, Kamati ilikutana kwa ajili tathimini ya utekelezaji wa ziara zake za kukagua miradi kwa mwaka 2018/2019.

Wednesday, May 29, 2019

TANZIA MAREKANI NA NYUMBANI TANZANIA


wanajumuiya wenzetu Asya Mwilima na Kate Mwilima wamefiwa na mama yao mzazi Bi Leyla Hawadhi Mwilima leo hapa New York kwenye hospitali ya Calvary Bronx. Mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho taarifa zaidi za mahali na muda zitafuata baadae. Kama ulivyoutaratibu wetu wa kufarijiana tunaweza kuwafariji wafiwa kwenye kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa mama yao; 


Asya Mwilima
 
347-377-1739

ADDRESS 
1987 Adam Clayton Powell Jr Blvd # 5A New York, NY 10026 btn 120 and 119th street

Tutazidi kufahamishana taarifa zaidi kadri tutakavyozipata. 


Kwa sasa tuzidi kumuombea marehemu Bi Leyla Mwilima Mwenyezi Mumgu ampokee peponi.


Innalillahi wainna ilayhi Rajiun.
Wabillah Tawfiq.


SEIF AKIDA
MWENYEKITI NYTC 


UPDATE ZA MSIBA WA MAMA YETU
Bi Leila Hawadhi Mwilima. 
Mazishi yatafanyika kesho tarehe 30/5/19


Harlem Islamic Community Center 
2001 7th Avenue corner of 120th street and 7th Avenue 
New York, NY-10027

Hii ni address ya mskiti ambao sala ya maiti itafanyika. Mwili wa marehemu unatarajiwa kufika mskitini saa tano asubuhi, then tutasalia maiti na baada ya hapo ndio tutaanza safari ya kwenda kuzika makaburi ya Malborough Muslim Cemetery in New Jersey

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA UONGOZI WA BUNGE LA VIJANA OFISINI KWAKE JIJINI DODOMA

  Spika wa Bunge, Job ndugai (kushoto) akisalimiana na Spika wa Bunge la Vijana 2018/2019, Ndg. Zephania Sane pale uongozi wa Bunge hilo ulipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge hilo, Ndg. Ashiruna Muhunzi  na katibu wa Bunge, Ndg. Alphonsina Ambrosi
Spika wa Bunge, Job ndugai (kushoto) akikabidhiwa ripoti ya Bunge la Vijana 2018/2019 na Spika wa Bunge hilo, Ndg. Zephania Sane alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

Spika wa Bunge, Job ndugai (Mwenye joho) akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Bunge la Vijana 2018/2019 ulipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Walioongozwa na Spika wa Bunge hilo, Ndg. Zephania Sane (wa nne kulia). (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA SHADA LA MAUA KATIKA MAKABURI YA MASHUJAA WA ZIMBABWE KATIKA ENEO LA NATIONAL HEROES ACRE WEST WING HARARE

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa mbele ya mnara wa Kumbukumbu ya Makaburi ya Mashujaa wa Taifa la Zimbabwe kabla ya kuweka shada la maua katika eneo hilo lililopo kilometa saba kutoka jiji la Harare nchini Zimbabwe.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiweka shada la maua mbele ya mnara wa Kumbukumbu ya Makaburi ya Mashujaa wa Taifa la Zimbabwe katika eneo hilo lililopo kilometa saba kutoka jiji la Harare nchini Zimbabwe.

MUFTI WA TANZANIA ASHIRIKI FUTARI ILIYOANDALIWA NA KIBADA GARDENS KIGAMBONI,ATOA NENO KWA WAGENI WAALIKWA

   Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally na Mh. Ali Davutoglu, Balozi wa Uturuki nchini Tanzania pamoja na baadhi ya wageni wakibadilishana mawazo kabla ya kufuturu.
     Muda wa Kufuturu (Iftar)

RC RUVUMA AFUNGUA SOKO LA MADINI TUNDURU

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme katikati akikata utepe kufungua soko la kuuzia Dhahabu na madini ya vito wilaya ya Tunduru kama utekelezaji wa agiza ka Rais Dkt John Magufuri aliloagiza kila wilaya na mkoa ambao una madini kufungua soko la kuuzia madini ambalo litawezesha wauzaji na wanunuzi kuuzia madini. Picha na Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Ruvuma
 Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme katikati akipiga makofi jana mara baada ya kukata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa soko la kuuzia Dhahabu na madini ya vito katika wilaya ya Tunduru mkoani humo,wa kwanza kushoto  mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru Mkwanda Sudi ,Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Sophia Kizigo na kulia Afisa madini Mkazi wa wilaya hiyo Juma Kapela.

Serikali inatambua Mchango wa Machifu katika Kulinda Mila na Desturi za Nchi

 Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza(kulia) akizungumza na Machifu kutoka Mkoa wa Singida na Mara Wilaya ya Rorya ambao walimtembelea ofisini kwake Mei 28 Jijini Dodoma kujadili masuala mbalimbali yanayohusu namna ya kuendeleza na kuhifadhi Mila na Desturi za nchi yetu.
 Mkurugenzi Idara ya Mendeleo ya Utamaduni Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Emmanuel Temu akizungumza  katika kikao cha Naibu Waziri Mhe Juliana Shonza (wa pili kulia) pamoja na Machifu wa Singida na Rorya kilichokua na lengo la kujadili namna ya kuendeleza na kuhifadhi Mila na Desturi za nchi yetu kilichofanyika Mei 28,Jijini Dodoma.

VIONGOZI NA WATUMISHI WA WIZARA YA MADINI WATAKIWA KUWA WAADILIFU KATIKA UTENDAJI KAZI WAO

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akifungua mafunzo ya viongozi wa Wizara ya Madini katika ukumbi wa St. Gaspar jijini Dodoma.
 Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya viongozi wa Wizara ya Madini wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,  Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) (hayupopichani) katika ukumbi wa St. Gaspar jijini Dodoma.

WAZIRI MKUU AWAFUTURISHA WATUMISHI WA OFISI YAKE


 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza katika futari aliyowaandalia watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Mei 28, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge , Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama baada ya futari aliyowaadalia watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Mei 28, 2019. Kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Bibi Maimuna Tarishi na wapili kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uwekezaji), Bibi Dorothy Mwaluko. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Tuesday, May 28, 2019

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS EMMERSON MNANGAGWA WA ZIMBWABWE

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Zimbabwe Mheshimiwa Emmerson Mnangagwa pamoja Mke wa Rais wa Zimbwabwe Amai Mnangagwa kabla ya kuanza mazungumzo katika Ikulu ya Harare Zimbabwe. Mei 28, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyeji wake Rais wa Zimbabwe Mheshimiwa Emmerson Mnangagwa Mnangagwa kabla ya kuanza mazungumzo katika Ikulu ya Harare Zimbabwe. Mei 28, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyeji wake Rais wa Zimbabwe Mheshimiwa Emmerson Mnangagwa, Mke wa Rais wa Zimbwabwe  Mhe. Amai Mnangagwa(Wapili kutoka kulia),Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Profesa Palamagamba Kabudi (Wapili kutoka kushoto),Waziri wa Mambo ya nje wa Zimbabwe Mhe.Sibusiso Moyo(Wakwanza kulia) pamoja na Mkuu wa Itifaki wa Tanzania  Balozi Grace Martin kabla ya kuanza mazungumzo katika Ikulu ya Harare Zimbabwe. Mei 28, 2019.

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA SHADA LA MAUA KATIKA MAKABURI YA MASHUJAA WA NCHI YA NAMIBIA KATIKA ENEO LA HEROES’ ACRE JIJINI WINDHOEK NAMIBIA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisali mbele ya Makaburi ya Mashujaa wa Namibia yaliyopo katika eneo la Heroes’ Acre mara baada ya kuweka shada la maua.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kuweka shada la maua katika Makaburi ya Mashujaa wa Namibia yaliyopo katika eneo la Heroes’ Acre mara baada ya kuwasili katika eneo hilo

WAZIRI MKUU AFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA AFYA NA VIONGOZI WA TAASISI YA AGA KHAN


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongoza mazungumzo kati yake, na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (wa pili kushoto) pamoja na Viongozi wa Taasisi ya Aga Khan, Ofisini kwa Waziri Mkuu, Bungeni jijini Dodoma, Mei 28, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameutaka uongozi wa Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan (AKDN) ukamilishe majadiliano yao na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuhusu matumizi ya kadi za NHIF kwenye hospitali zao ili Watanzania wengi zaidi waweze kunufaika.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Mei 28, 2019) alipokutana na viongozi kadhaa wa taasisi hiyo pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, ofisini kwake bungeni jijini Dodoma.

Waziri Mkuu amesema Serikali inatambua mchango unaotolewa na taasisi ya AKDN katika kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya.“Nilijionea kazi kazi kubwa inayofanyika pale Hospitali ya Aga Khan Machi, mwaka huu, niliongea na wagonjwa na kupata maoni yao, lakini kikubwa tu mpunguze gharama na muimarishe huduma zenu,” amesema.

NAIBU SPIKA AICHANGIA YANGA

 Naibu Spika  Dkt Tulia Ackson akikabidhi fedha kiasi cha Shilingi milioni moja kwa Wabunge mashabiki wa Timu ya Soka ya Yanga iliyopokelewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mheshimiwa Anthony Mavunde, Ofisini kwake Bungeni mjini Dodoma. Fedha hizo ni kwa ajili ya kuichangia Timu ya Yanga.
 Naibu Spika  Dkt Tulia Ackson akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi fedha kiasi cha Shilingi milioni moja kwa Wabunge mashabiki wa Timu ya Soka ya Yanga kwa ajili ya kuichangia timu hiyo, Ofisini kwake Bungeni mjini Dodoma .

(PICHA NAOFISI YA BUNGE)
   

MBWANA SAMATTA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MSEMAJI MKUU WA SERIKALI, DKT. HASSAN ABAASI

 Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimkabidhi jarida la Nchi Yetu Tanzania, Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) anayekipiga katika Klabu ya KRC Genk ya Nchini Ublegiji Mbwana Samatta amara baada ya mazungumzo baina yao katika Ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jumanne (Mei 28, 2019) Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, (wa tatu kulia) Dkt. Hassan Abbasi akiwa katika picha ya pamoja na Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na Mshambuaji wa Klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji (katikati) mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo baina yao katika Ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO leo Jumanne (Mei 28, 2019) Jijini Dar es Salaam.

NAIBU SPIKA AKUTANA NA MKURUGENZI UNDP

Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Ndugu Verity Nyagah alipomtembelea ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. 

PITA PITA YA VIJIMABOBLOG BAKU, AZERBAIJAN EUFA EUROPA FINAL 2019


Vijimambo live ndani ya final ya EUFA EUROPA kati ya Chelsea na Arsenal,Baku Olympic Stadium, Azerbaijani uwaanja wenye uwezo wa kubeba watazamaji 69,870 ni kati ya viwanja vikubwa na maarufu vya mpira wa miguu duniani.


Ulinzi kama wote polisi wenye mbwa tayari kukalibiana na washabiki wa Uingereza zinakotoka timu hizi maili, UK kunasifa za washabiki wenye fujo duniani hasa linavyokuja swala la mchezo wa mpira wa miguu.


Hapa ni Park  maalumu itakayotumia na shamla shamla za ufunguzi wa final hizo.



Baku pia ni maarufu sana kwa mchezo wa magari  ya kasi yajulikanayo kama Formula 1
,The FIA Formula One World kwaiyo hapa ni park iliyopewa jina la Formula 1 Park na inavibao vya washiriki wote wa mashindano hayo ya magari yaendayo kasi.  Na 2020 june kutafanyika mshindani hayo ndani ya jiji hili la Baku.

Ny Ebra kutoka New York, USA hadi Baku kushuhudia final hizo za EUROPA akiwa kama mnazi wa Arsenal. Akipata ukodak na wenyeji  wake. Kwa picha zaidi nenda chini kiroho safi.